پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · At-Tawba
سورهٔ ۹

At-Tawba

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۹۹

وَمِنَ ٱلْأَعْرَابِ مَن يُؤْمِنُ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ وَيَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ قُرُبَـٰتٍ عِندَ ٱللَّهِ وَصَلَوَٰتِ ٱلرَّسُولِ ۚ أَلَآ إِنَّهَا قُرْبَةٌ لَّهُمْ ۚ سَيُدْخِلُهُمُ ٱللَّهُ فِى رَحْمَتِهِۦٓ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ۹۹

{99} Si mabedui wote wenye kulaumiwa, bali wamo miongoni mwao “kuna yule anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho,” kwa hivyo akasalimika kwa hayo kutokana na ukafiri na unafiki, na anatenda kwa mujibu wa Imani. “Na anakichukulia kile anachotoa kuwa ni cha kuwasogeza karibu kwa Mwenyezi Mungu;” yaani, anatarajia matumizi yake anayotoa, na anakusudia kwayo uso wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kujiweka karibu naye, "na" anayafanya kuwa ni njia ya kupatia dua za "Mtume." Yaani, dua yake juu yao na baraka zake juu yao. Amesema Yeye Mtukufu, akibainisha manufaa ya dua za Mtume: "Ndiyo! Hizo hakika ni mambo ya kuwasogeza wao karibu” na Mwenyezi Mungu, na zinawazidishia mali zao, na zinaingiza baraka humo. "Mwenyezi Mungu atawaingiza katika rehema yake” miongoni mwa mwa waja wake wema. Hakika Yeye ni “Mwenye kusitiri dhambi, Mwenye kurehemu.” Anasitiri mabaya makubwa ya wale wanaotubia kwake, na amewajumuisha waja wake kwa rehema yake ambayo ilienea kila kitu, na anawateua waja wake Waumini kwa rehema anayowawezesha kwayo kufanya mema, na anawalinda ndani yake kutokana na kufanya ukiukaji, na anawalipa ndani yake kwa aina nyingi mbalimbali za malipo. Na katika Aya hii kuna ushahidi kwamba Mabedui ni kama watu wa mjini. Miongoni mwao wapo wanaosifiwa, na miongoni mwao wapo wanaokashifiwa. Na Mwenyezi Mungu hakuwashutumu kwa sababu ya ubedui wao na kukaa kwao jangwani tu; bali aliwashutumu kwa kuacha maamrisho ya Mwenyezi Mungu, na kwamba wako katika uwezekano mkubwa wa hilo. Na miongoni mwake ni kwamba ukafiri na unafiki huongezeka, na hupungua, na huwa mgumu, na hufifia kulingana na hali mbalimbali. Na miongoni mwake ni ubora wa elimu, na kwamba aliyeikosa yuko karibu zaidi na uovu kuliko anayeijua. Kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwashutumu Mabedui, na akajulisha kuwa wao wana ukafiri mkubwa zaidi na unafiki, na akataja sababu yenye kuleta hayo, na kwamba wameelekea zaidi kutojua mipaka ya yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu juu ya Mtume wake. Na miongoni mwake ni kwamba elimu yenye manufaa, ambayo ndiyo elimu yenye manufaa zaidi ni kujua mipaka ya yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake miongoni mwa misingi ya dini na matawi yake kama vile kujua mipaka ya imani, na Uislamu, na ihsan, na uchamungu, na kufaulu, na utiifu, na wema, na kuunga jamaa, na kufanya uzuri, na ukafiri, na unafiki, na kuvuka mipaka, na uasi, na uzinzi, na pombe, na riba na mfano wa hayo. Kwa maana katika kuyajua mtu anakuwa na uwezo wa kuyafanya ikiwa yameamrishwa au kutoyafanya ikiwa yameharamishwa, na kuyaamrisha au kuyakataza. Na miongoni mwake ni kwamba Muumini anapaswa kutekeleza yale yaliyo ya wajibu juu yake miongoni mwa haki mbalimbali, na kwa kifua kikunjufu, kwa nafsi tulivu, akiwania kwamba yawe ya faida na si ya hasara.