At-Tawba
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَٱلسَّـٰبِقُونَ ٱلْأَوَّلُونَ مِنَ ٱلْمُهَـٰجِرِينَ وَٱلْأَنصَارِ وَٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوهُم بِإِحْسَـٰنٍ رَّضِىَ ٱللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا۟ عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّـٰتٍ تَجْرِى تَحْتَهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ خَـٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ ۱۰۰
{100} Waliotangulia ni wale waliotangulia umma huu na wakautangulia kuharashika kuamini, na kuhama, na jihadi, na kuisimamisha Dini ya Mwenyezi Mungu, "katika Wahajiri," "waliotolewa majumbani mwao na mali yao kwa ajili ya kutafuta fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi zake, na wanamsaidia Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao ndio wakweli.” "Na" katika "Ansar;" "walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda wale waliohamia kwao, wala hawaoni uchoyo katika vifua vyao kwa vile walivyopewa (Wahajiri), bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji.” "Na wale waliowafuata kwa uzuri” kwa itikadi, na kauli, na matendo. Basi hawa ndio waliosalimika na shutuma, na wakapata sifa ya juu zaidi na utukufu bora zaidi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. "Mwenyezi Mungu aliwaridhia” na ridha yake Yeye Mtukufu ni kubwa zaidi kuliko neema ya Peponi. "Na wao walimridhia, na amewaandalia Bustani zipitazo mito chini yake” ambayo inapelekwa ili kwenda kuzinywesha bustani na makonde yenye kung'aa, zenye maua, na bustani nzuri. "Watadumu humo milele." Hawatatafuta kutoka humo, wala hawataomba badala yake kitu. Kwa sababu chochote wanachotamani wanakipata, na chochote wanachotaka wanakipata. "Huko ndiko kufuzu kukubwa” ambako walipata kuna kila kitu kinachopendwa na nafsi, na raha kwa roho, na neema kwa mioyo, na matamanio kwa miili, na wakazuilika na kila kinachoepukwa.