At-Tawba
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَمِنَ ٱلْأَعْرَابِ مَن يَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ مَغْرَمًا وَيَتَرَبَّصُ بِكُمُ ٱلدَّوَآئِرَ ۚ عَلَيْهِمْ دَآئِرَةُ ٱلسَّوْءِ ۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ۹۸
{98} Miongoni mwa hayo ni kwamba, Mabedui wana uchoyo mkubwa juu ya mali na ni mabahili zaidi juu yake. Kwa hivyo, miongoni mwao “kuna yule anayefikiri kile wanachotoa” miongoni mwa Zaka na masurufu katika njia ya Mwenyezi Mungu na mengineyo, "kuwa ni gharama ya bure." Yaani, anayaona kuwa ni hasara na upungufu, wala hatarajii malipo juu yake, wala hataki uso wa Mwenyezi Mungu kwa hilo, wala hakaribii kutoa isipokuwa kwa kulazimishwa. "Na anawatazamia nyinyi mambo yawageukie;” yaani, katika uadui wao kwa Waumini na chuki yao juu yao ni kwamba wanapenda na wanangojelea mambo ya nyakati yawageukie na misiba yake. Lakini hili litawageukia wao, kwani “Mageuko maovu yatakuwa juu yao!” Ama Waumini, wao wana mzunguzo mzuri wa mambo dhdii ya maadui zao, nao wana mwisho mzuri. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote.” Anayajua makusudio ya waja wake na kilichoyafanya matendo kutokea miongoni mwa ikhlasi na mengineyo.