Al-An'aam
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
فَكُلُوا۟ مِمَّا ذُكِرَ ٱسْمُ ٱللَّهِ عَلَيْهِ إِن كُنتُم بِـَٔايَـٰتِهِۦ مُؤْمِنِينَ ۱۱۸ وَمَا لَكُمْ أَلَّا تَأْكُلُوا۟ مِمَّا ذُكِرَ ٱسْمُ ٱللَّهِ عَلَيْهِ وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا ٱضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ ۗ وَإِنَّ كَثِيرًا لَّيُضِلُّونَ بِأَهْوَآئِهِم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِٱلْمُعْتَدِينَ ۱۱۹
{118 - 119} Yeye Mtukufu anawaamrisha waja wake Waumini kulingana na matakwa ya imani, na kwamba ikiwa ni Waumini, Basi na wale waliotajiwa jina la Mwenyezi Mungu miongoni mwa mifugo na wanyama wengineo walio halali, na waitakidi uhalali wake, na wala wasifanye kama wanavyofanya watu wa zama za Ujinga kwa kuharamisha mengi ya halali kwa kuzua hilo wao wenyewe, na kwa sababu ya kupotoshwa na mashetani wao. Kwa hivyo mwenyezi Mungu akataja kuwa alama ya Muumini ni kuwahalifu watu wa zama za Ujinga katika ada hii inayoshutumiwa, inayojumuisha kubadilisha sheria ya Mwenyezi Mungu, na kwamba ni kitu gani kinachowazuia kula katika kile kilichotajiwa jina la mwenyezi Mungu, na tayari Mwenyezi Mungu alikwisha waelezea kwa kina waja wake vile alivyowaharimishia, na akavibainisha, na akaviweka wazi. Kwa hivyo hakuna tatizo lolote wala shaka yoyote iliyobaki ndani yake inayomtaka mtu ajizuie kula baadhi ya vilivyo halali kwa kuhofia kuingia katika haramu. Na Aya hii tukufu iliashiria kwamba kanuni ya msingi katika vitu na vyakula ni kwamba vinaruhusiwa, na kwamba ikiwa sheria haijaleta uharamisho wa kitu katika hivyo, basi vinabakia kuwa vinaruhusiwa. Kwa hivyo vile ambavyo Mwenyezi Mungu alivinyamazia, basi hivyo vinaruhusiwa. Kwa sababu haramu Mwenyezi Mungu amekwisha ieleza kwa kina, na kile ambacho hakunieleza kwa kina, basi hicho si haramu. Lakini pamoja na hayo, haramu ambayo Mwenyezi Mungu aliieleza kwa kina na akaiweka wazi, aliiruhusu katika hali ya dharura, na shida kubwa, Kama alivyosema Yeye Mtukufu: "Mmeharimishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe..." mpaka aliposema; "Lakini aliyefikiwa na dharura bila ya kutamani wala kupita kiasi, yeye hana dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu." Kisha akaonya juu ya wengi katika watu, akasema: "Na hakika wengi wanapoteza kwa matamanio yao." Yaani, kwa yale tu ambayo nafsi zao zinayatamani "bila ya kuwa na elimu," wala hoja. Basi mja ajihadhari na mfano wa hawa, , na alama zao ni kama Mwenyezi Mungu alivyowaelezea waja wake kuwahusu, kwamba wito wao haujengeki juu ya ushahidi wowote wala hawana hoja yoyote ya kisheria. Lakini wana fikira potofu kulingana na matamanio yao maovu, na maoni yao yenye upungufu. Basi hawa wameivuka sheria ya Mwenyezi Mungu na dhidi ya waja wa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu hawapendi wavukao mipaka. Tofauti na waongoao, waongofu. Wao wanalingania kwenye haki na uwongofu, na wanauunga mkono wito wao kwa hoja za kiakili na za kimaandiko, na wala hawafuati katika wito wao isipokuwa ridhaa ya Mola wao Mlezi na kujiweka karibu naye.