Al-An'aam
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَذَرُوا۟ ظَـٰهِرَ ٱلْإِثْمِ وَبَاطِنَهُۥٓ ۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَكْسِبُونَ ٱلْإِثْمَ سَيُجْزَوْنَ بِمَا كَانُوا۟ يَقْتَرِفُونَ ۱۲۰
{120} Kinachomaanishwa na dhambi ni maasia yote ambayo yanamfanya mja kuwa na dhambi. Yaani, kuingia kwake katika dhambi na ubaya ni katika mambo yanayohusiana na haki za Mwenyezi Mungu, na haki za waja wake, basi Mwenyezi Mungu akawakataza waja wake kufanya dhambi ya dhahiri, na ile iliyofichika. Yaani, ya siri na ya wazi, zinazohusiana na mwili na viungo, na kuhusiana na moyo. Na wala mja hawezi kuacha kabisa maasia ya dhahiri na yaliyofichika isipokuwa baada ya kuyajua na kutafuta kuyajua. Kwa hivyo kunakuwa kutafuta kuyajua na kuyajua maasia ya moyo, na mwili, na kuyajua hayo ni wajibu kwa yule anayewajibishwa na sheria. Na wengi katika watu dhambi nyingi zimefichwa kwake, hasa dhambi za moyo, Kama vile kiburi, kujifahiri, na riyaa ... na mfano wa hayo, mpaka akawa na mengi katika hayo hali ya kuwa hahisi wala hatambui. Na hilo ni katika kuipa mgongo elimu na kutokuwa na utambuzi. Kisha Yeye Mtukufu akajulisha kwamba wale wanaochuma madhambi yaliyo dhahiri na yaliyofichika, watalipwa kulingana na kuchuma kwao, na kwa kiasi cha madhambi yao, yawe machache au mengi. Na malipo haya yatakuwa katika Akhera, na huenda yakawa katika dunia hii. Mja anaadhibiwa, kwa hivyo anahafifishiwa hilo katika mabaya yake.