Al-Baqara
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ سَوَآءٌ عَلَيْهِمْ ءَأَنذَرْتَهُمْ أَمْ لَمْ تُنذِرْهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ 6
Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kwamba, “Hakika wale waliokufuru", yani wanaosifika kwa ukafiri, na wakajipaka ukafiri, na ukawa sifa ya lazima kwao, na hakuna kemeo lolote linaloweza kuwazuia kutokana nao, na wala mawaidha hayawezi kuwaingia; na kwamba wao wanaendelea katika ukafiri wao. Kwa hivyo, ni sawa kwao "ukiwaonya au usiwaonye, hawaamini." Na uhakika wa ukafiri ni kukataa aliyokuja nayo Mtume au kukataa baadhi yake. Kwa hivyo, makafiri hao hauwafaidi ulinganizi (kwa Mwenyezi Mungu) isipokuwa tu kwa ajili ya kusimamishia hoja juu yao. Na ni kana kwamba katika hili kuna kukata matumaini ya Mtume - rehema na amani ziwe juu yake - katika kuamini kwao. Kwa hivyo, usiwe na huzuni juu yao, wala nafsi yako isijihiliki kwa kuwasikitikia.