Al-Baqara
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
خَتَمَ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَعَلَىٰ سَمْعِهِمْ ۖ وَعَلَىٰٓ أَبْصَـٰرِهِمْ غِشَـٰوَةٌ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ 7
Kisha akataja vizuizi vinavyowazuia kuamini, akasema:
(7) “Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao, na juu ya masikio yao.” Yaani, amepiga juu yake kwa chapa ambazo imani haiwezi kuingia ndani yake, wala haiwezi kupita ndani yake. Kwa hivyo, hawaelewi kuelewa kwa kuwanufaisha, na wala hawasikii kusikia kwa kuwafaidi. “Na juu ya macho yao pana pazia,” yaani pazia, kifuniko, na kizuizi, ambavyo vinayazuia (macho) wasione kuona kwa kuwanufaisha. Na hizi ndizo njia za elimu na heri ambazo wameshafungiwa, kwa hivyo hakuna matumaini yoyote juu yao, wala haitarajiwi heri yoyote kwao. Na kwa hakika, walizuiwa hayo, na wakafungiwa milango ya imani kwa sababu ya ukafiri wao, na kukataa kwao, na upinzani wao baada ya haki kuwabainikia, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Nasi twazigeuza nyoyo zao na macho yao kama walivyokuwa hawakuamini mara ya kwanza;” na hii ni adhabu ya haraka. Kisha akataja adhabu ya baadaye, akasema: “Basi watapata adhabu kubwa.” Nayo ni adhabu ya Motoni, na ghadhabu ya Al-Jabbar (afanyaye atakalo) yenye kuendelea, yenye kudumu.