Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sura ya 2

Al-Baqara

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 58

وَإِذْ قُلْنَا ٱدْخُلُوا۟ هَـٰذِهِ ٱلْقَرْيَةَ فَكُلُوا۟ مِنْهَا حَيْثُ شِئْتُمْ رَغَدًا وَٱدْخُلُوا۟ ٱلْبَابَ سُجَّدًا وَقُولُوا۟ حِطَّةٌ نَّغْفِرْ لَكُمْ خَطَـٰيَـٰكُمْ ۚ وَسَنَزِيدُ ٱلْمُحْسِنِينَ 58

(58) Na hii pia ni katika neema zake juu yao baada ya kumuasi Yeye. Basi akawaamrisha waingie katika mji ambao humo watakuwa na utukufu, na nchi na makazi. Na watapata humo riziki nyingi. Na kwamba kuingia kwao kuwe kwa namna ambayo kwayo watamnyenyekea Mwenyezi Mungu kwa vitendo, nako ni kuingia mlangoni kwa kusujudu, yani kwa unyenyekevu na udhalilifu. Na kwa kauli, ambayo ni kusema: "Tusamehe!" Yani kuwasamehe dhambi zao kwa wao kumuomba Yeye msamaha. "Tutakusameheni makosa yenu" kwa kuomba kwenu msamaha, "na tutawazidishia wema wafanyao wema." Kwa vitendo vyao, yani kuwalipa malipo ya haraka na ya baadaye.