پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · At-Tawba
سورهٔ ۹

At-Tawba

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۷۸

أَلَمْ يَعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ يَعْلَمُ سِرَّهُمْ وَنَجْوَىٰهُمْ وَأَنَّ ٱللَّهَ عَلَّـٰمُ ٱلْغُيُوبِ ۷۸

{78} Na ndiyo maana akamuahidi adhabu yule aliyefanya miongoni mwao kitendo hiki, kwa kauli yake, "Je, hawajui kwamba Mwenyezi Mungu anajua siri zao na minong'ono yao, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyajua sana ya ghaibu?" Na atawalipa kwa matendo waliyoyafanya ambayo Mwenyezi Mungu anayajua. Na Aya hizi ziliteremka kuhusiana na mwanamume mmoja miongoni mwa wanafiki aliyeitwa Tha'labah. Alimjia Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimfikie - na akamuomba amuombee kwa Mwenyezi Mungu ili Mwenyezi Mungu ampe katika fadhila yake, na kwamba ikiwa atampa, bila shaka atatoa sadaka, na kuunga jamaa, na kusaidia katika kukabiliana na misiba ya haki. Basi Nabii -rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimfikie - akamuombea, kwa hivyo akawa na kondoo, na hawakuacha kuongezeka mpaka akatoka nao nje ya Madina. Kwa hivyo akawa haji isipokuwa katika baadhi ya Swala tano tu. Kisha akaenda mbali, na akawa haji isipokuwa katika Swala ya Ijumaa tu. Kisha wakawa wengi, basi akawapeleka mbali, kwa hivyo akawa haji si katika Swalah ya Ijumaa wala Swala ya jamaa. Kwa hivyo, Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimfikie - akamkosa, na akajulishwa hali yake. Basi akatuma wenye kuchukua sadaka kutoka kwa wenyewe, na wakapita karibu na Tha'labah, akasema. “Hawa si chochote isipokuwa ni jizyah. Hawa si chochote isipokuwa dada wa jizyah." Basi pindi hakuwapa, wakaja na wakamjulisha Nabii – rehema na amani ziwe juu yake – juu ya hili, naye akasema, “Ole wake Tha'laba. Ole wake Tha'laba!" Mara tatu. Kwa hivyo, aya hii ilipoteremka kumhusu yeye na mfano wake, baadhi ya jamaa zake wakamwendea nayo, na wakaifikisha kwake. Basi akaja na zaka yake, lakini Nabii - rehema na amani zimshukie - hakuikubali. Kisha akaja nayo kwa Abu Bakr baada ya kufariki kwa Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - lakini hakuikubali. Kisha akaja nayo baada ya Abu Bakr kwa Umar, naye hakuikubali. Basi inasemwa kwamba aliangamia wakati wa uongozi wa Uthman.