Al-An'aam
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
ثُمَّ رُدُّوٓا۟ إِلَى ٱللَّهِ مَوْلَىٰهُمُ ٱلْحَقِّ ۚ أَلَا لَهُ ٱلْحُكْمُ وَهُوَ أَسْرَعُ ٱلْحَـٰسِبِينَ ۶۲
{62} "Kisha," baada ya kufa, na uhai wa Barzakh (kaburini) na yaliyomo ya kheri na shari, "watarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, Mola wao wa Haki ." Yaani, ambaye aliwasimamia kwa hukumu yake ya kimajaliwa, na akawatekelezea aina zote za uendeshaji Aliotaka. Kisha akawasimamia kwa maamrisho yake na makatazo yake, na akawatumia Mitume na akawateremshia Vitabu; kisha wakarudishwa Kwake ili awasimamie katika kuwahukumu kwa malipo. Na Awalipe juu ya yale waliyoyafanya miongoni mwa mema na awaadhibu kwa maovu na mabaya. Na ndiyo maana Akasema, "Hakika, hukumu ni yake," peke yake bila ya mshirika; "Naye ni Mwepesi kuliko wote wanaohesabu." Kwa sababu ya ukamilifu wa elimu yake na kuhifadhi kwake matendo yao, kulingana na Aliyoyaandika katika Ubao Uliohifadhiwa; kisha Malaika Wake wakayaandika katika Kitabu ambacho kiko katika mikono yao. basi ikiwa Mwenyezi Mungu ndiye wa peke Yake katika kuumba na kuenda kwa mambo, na Yeye ndiye Mwenye nguvu ya ushindi juu ya waja Wake, na Amewachunga sana katika hali zao zote. Na Yeye ndiye Mwenye hukumu ya kimajaliwa, na hukumu ya kisheria, na hukumu ya kimalipo. Basi ni vipi washirikina wanaweza kumwacha yule ambaye hizi ndizo sifa zake na maelezo yake na wakamuabudu yule asiyekuwa na chochote katika mambo haya, wala hana uzito wa chembe ya manufaa, wala hana uwezo na utashi. Basi ninaapa kwa Mwenyezi Mungu; lau wangejua upole wa Mwenyezi Mungu juu yao, na usamehevu wake na rehema yake kwao; ilhali wao wanapigana naye kwa ushirikina na ukafiri, na wanafanya ujasiri katika kuukana ukuu wake kwa uwongo na uzushi, na hali Yeye anawapa salama, na anawaruzuku. Basi misukumo yao ingevutika katika kumjua Yeye, na akili zao zingestaajabishwa na kumpenda yeye, na wangejichukia wenyewe kwa chuki kubwa zaidi kwa kuwa waliufuata msukumo wa Shetani; ambao unaleta hizaya na hasara; lakini wao ni kaumu wasiotumia akili.