پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-An'aam
سورهٔ ۶

Al-An'aam

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۱۴۳

ثَمَـٰنِيَةَ أَزْوَٰجٍ ۖ مِّنَ ٱلضَّأْنِ ٱثْنَيْنِ وَمِنَ ٱلْمَعْزِ ٱثْنَيْنِ ۗ قُلْ ءَآلذَّكَرَيْنِ حَرَّمَ أَمِ ٱلْأُنثَيَيْنِ أَمَّا ٱشْتَمَلَتْ عَلَيْهِ أَرْحَامُ ٱلْأُنثَيَيْنِ ۖ نَبِّـُٔونِى بِعِلْمٍ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ ۱۴۳

{143} Na hawa mifugo ambao Mwenyezi Mungu aliwaneemesha kwao juu ya waja wake, na akawafanya wote kuwa halali na wazuri, aliwaeleza kwa kina kwamba ni: "majozi manane: katika kondoo ni wawili", dume na jike, "na katika mbuzi ni wawili" vile vile. Basi hawa ni wanne, wote wanaingia katika yale aliyohalalisha Mwenyezi Mungu, na hakuna tofauti baina yeyote katika hao. Basi waambie hawa wanaojitia katika ugumu, ambao wanaharamisha katika hao baadhi yao na kuacha baadhi yao, au wanawaharamisha baadhi yao kwa wanawake na sio kwa wanaume, ukiwalazimisha kuwa hakuna tafauti baina ya wale waliowaruhusu katika hao na wale waliowaharamisha: "Je, madume wawili hawa" katika kondoo na mbuzi ndiyo "ameharamisha" Mwenyezi Mungu? Lakini nyinyi hamsemi hivyo katika hali zote. "Majike wawili hawa," Mwenyezi Mungu aliharamisha katika kondoo na mbuzi. Lakini kauli yenu si hii. Si kuharamisha madume wote wawili, wala majike wote wawili katika aina mbili hizi. Na inabaki ikiwa tumbo lunajumuisha dume na jike au kisichojulikana. Basi akasema, "au" mnaharamisha "wale waliomo matumboni mwa majike yote mawili haya?" Yaani, kondoo jike na mbuzi jike, bila ya tofauti yoyote kati ya dume na jike. Lakini nyinyi pia hamsemi kauli hii. Kwa hivyo ikiwa hamsemi kwa mojawapo ya kauli hizi tatu ambazo zimefungia kategoria zinazowezekana katika hao, basi mnaenda kwa kitu gani? "Niambieni kwa elimu ikiwa nyinyi ni wakweli" katika kauli yenu hiyo na madai yenu. Na inajulikana kuwa hawawezi kusema kauli yenye kuingia katika akili isipokuwa moja katika hizi tatu, lakini wao hawasemi hata mmoja katika hizi. Bali wanasema, hakika baadhi ya mifugo ambao wanakubaliana juu yake kukubaliana kwao wenyewe tu ni haramu kwa wanawake na si kwa wanaume, au ni haramu katika wakati fulani miongoni mwa nyakati. Au mfano wa hayo miongoni mwa kauli ambazo anajulikana kwa elimu isiyokuwa na shaka ndani yake kwamba chanzo chake ni kwa sababu ya ujinga uliopandana, na akili mbaya, potofu, na maoni mabovu, na kwamba Mwenyezi Mungu hakuyateremshia yale waliyoyasema mamlaka yoyote, wala hawana hoja yoyote juu yake wala ushahidi.