Al-An'aam
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَقَالُوا۟ مَا فِى بُطُونِ هَـٰذِهِ ٱلْأَنْعَـٰمِ خَالِصَةٌ لِّذُكُورِنَا وَمُحَرَّمٌ عَلَىٰٓ أَزْوَٰجِنَا ۖ وَإِن يَكُن مَّيْتَةً فَهُمْ فِيهِ شُرَكَآءُ ۚ سَيَجْزِيهِمْ وَصْفَهُمْ ۚ إِنَّهُۥ حَكِيمٌ عَلِيمٌ ۱۳۹
{139} Na miongoni mwa maoni yao ya kipuuzi ni kwamba wanawafanya baadhi ya mifugo na wanawatenga wakiharamisha vilivyomo matumboni mwao juu ya wanawake na si wanaume. Na wanasema: "Vile vilivyo katika matumbo ya mifugo hawa ni ya wanaume wetu tu." Yaani, ni halali kwao, na wala wanawake hawashiriki ndani yake. "Na vimeharimishwa kwa wake zetu;" yaani, wanawake wetu. Na hili ni ikiwa atazaliwa hai. Na ikiwa kilicho ndani ya tumbo lake ni mfu, basi wao ni washirika ndani yake. Yaani, ni halali kwa wanaume na wanawake. "Atawalipa," yaani, Mwenyezi Mungu "maelezo yao hayo" ambapo waliyaeleza yale aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu kuwa ni haramu, na wakaieleza hatamu kuwa ni halali; basi wakaipinga sheria ya Mwenyezi Mungu, na wakaihalifu, na wakalinasibisha hilo kwa Mwenyezi Mungu. "Hakika Yeye ni Mwenye hekima kubwa." Ambapo aliwapa muhula, na akawawezesha kuwa katika hali yao hiyo ya upotevu. "Mwenye kujua vyema" hali yao, na hakifichikani kwake chenye kufichikana. Naye Mtukufu anawajua, na yale waliyoyasema juu Yake, na wakazua ya uongo; naye anawapa salama, na Anawaruzuku Yeye Utukufu mkubwa.