پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-An'aam
سورهٔ ۶

Al-An'aam

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۱۲

قُل لِّمَن مَّا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۖ قُل لِّلَّهِ ۚ كَتَبَ عَلَىٰ نَفْسِهِ ٱلرَّحْمَةَ ۚ لَيَجْمَعَنَّكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ ٱلْقِيَـٰمَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ ۚ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ۱۲

{12} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake - rehema na amani zimshukie - "Sema" washirikina hawa [kwa Mwenyezi Mungu] ukiwafanya kukukiri, na ukiwafanya wailazimu Tauhidi: Ni vya nani vilivyo katika mbingu na katika ardhi?" Yaani, ni nani Muumba wa hivyo, Mmiliki wake, Mwenye kuviendesha? "Sema," ukiwaambia, "Ni vya Mwenyezi Mungu," nao wanakiri hilo wala hawalikanushi. Je, kwa nini wanapomkiria Mwenyezi Mungu upweke katika ufalme na kuendesha mambo, hawakumkiria pia kumfanyia mambo kwa ikhlas na kumuabudu Yeye tu. "Yeye ameiandika rehemu juu ya nafsi yake;" Yaani, ulimwengu wa juu na wa chini uko chini ya ufalme wake na uendeshaji Wake. Naye Mtukufu amewakunjulia rehema zake na ihsan yake, na akawafunika kwa rehema zake na neema zake; na akajiandikia andiko kwamba rehema yake inashinda ghadhabu yake. Na kwamba, kutoa ni kupendeza zaidi Kwake kuliko kuzuilia, na kwamba Mwenyezi Mungu amewafungulia waja wake wote milango ya rehema ikiwa hawataifunga wenyewe milango yake kwa dhambi zao, na akawaita kwayo ikiwa dhambi zao na makosa hayatawazuia kuitafuta. Na kauli yake, "Hakika atawakusanya hadi Siku ya Qiyama isiyokuwa na shaka."Na hiki ni kiapo kutoka kwake, na Yeye ndiye Mkweli zaidi wa watoa habari. Na amesimamisha juu ya hayo hoja na ushahidi yenye kuyafanya kuwa yakini ya uhakika, lakini madhalimu walikataa isipokuwa kukanusha tu. Na wakakanusha uwezo wa Mwenyezi Mungu wa kufufuliwa kwa viumbe, kwa hivyo wakaanguka katika kumuasi, wakafanya ujasiri juu ya kumkufuru Yeye. Kwa hivyo wanahasiri dunia yao na akhera yao, na ndiyo maana akasema; "Wale waliojihasiri nafsi zao, wao hawaamini."