Al-Qamar
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
أَءُلْقِىَ ٱلذِّكْرُ عَلَيْهِ مِنۢ بَيْنِنَا بَلْ هُوَ كَذَّابٌ أَشِرٌ ۲۵ سَيَعْلَمُونَ غَدًا مَّنِ ٱلْكَذَّابُ ٱلْأَشِرُ ۲۶
{25 - 26} "Ni yeye tu aliyeteremshiwa huo ukumbusho kati yetu sote?" Yaani, vipi Mwenyezi Mungu anamchangua yeye tu miongoni mwetu na kumteremshia ukumbusho? Ni sifa gani maalumu aliyo nayo inayomtofautisha na sisi? Na hili ni pingamizi kutoka kwa wale wanaomkadhibisha Mwenyezi Mungu ambalo wameendelea kulitumia na kulitetea na kukataa kwalo wito wa Mitume, lakini Mwenyezi Mungu alijibu fikira hii potofu kwa kauli ya Mitume kwa watu wao, "Mitume wao wakawaambia: 'Sisi kweli si chochote ila ni wanadamu kama nyinyi. Lakini Mwenyezi Mungu humfanyia hisani amtakaye katika waja wake.'" Basi Mitume wamepewa neema na Mwenyezi Mungu za sifa, na maadili, na mambo ya ukamilifu ambayo kwayo waliufailia kufanywa kuwa mitume wa Mola wao Mlezi, na kupewa wao tu Ufunuo wake, na ni kutokana na rehema zake na hekima yake kwamba walikuwa ni wanadamu. Kama wangelikuwa katika malaika, isingekuwa rahisi kwa wanadamu kupokea kutoka kwao. Na kama angewafanya kuwa ni wa kutoka katika malaika, basi angewaharakishia wale wanaowakadhibisha adhabu. Na lengo la maneno haya yaliyotoka kwa Thamudi wakimwambia Nabii wao Saleh ni kumkadhibisha, na ndiyo maana wakamhukumu kwa hukumu hii isiyo ya haki, wakasema: "Bali huyu ni mwongo mno mwenye mshari mkubwa!" Mwenyezi Mungu awaangamize! Ni wapumbavu namna gani hawa katika maono yao, na dhalimu wakubwa namna gani, na wabaya zaidi namna gani katika kupinga wakweli na wanyoofu kwa maneno mabaya zaidi.