Qaaf
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
تَبْصِرَةً وَذِكْرَىٰ لِكُلِّ عَبْدٍ مُّنِيبٍ ۸ وَنَزَّلْنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً مُّبَـٰرَكًا فَأَنۢبَتْنَا بِهِۦ جَنَّـٰتٍ وَحَبَّ ٱلْحَصِيدِ ۹ وَٱلنَّخْلَ بَاسِقَـٰتٍ لَّهَا طَلْعٌ نَّضِيدٌ ۱۰ رِّزْقًا لِّلْعِبَادِ ۖ وَأَحْيَيْنَا بِهِۦ بَلْدَةً مَّيْتًا ۚ كَذَٰلِكَ ٱلْخُرُوجُ ۱۱
{8 - 11} Miongoni mwa manufaa hayo, alizitaja kwa njia mahususi bustani zenye matunda matamu kama vile zabibu, mikomamanga, michungwa, tufaha na aina nyinginezo za matunda, na mitende mikubwa, ambayo manufaa yake ni marefu, na inamea ikaenda juu mpaka ikafikia urefu ambao miti mingi haifiki. Kisha ikatoa makole yaliyozaa kwa wingi katika mashada yake vitu ambavyo ni riziki ya waja, chakula kikuu, vitoweo, na matunda wanayokula na kujiwekea akiba wao na mifugo yao. Na vile vile anachokitoa Mwenyezi Mungu kwa mvua, na matokeo yake kama vile mito iliyo juu ya uso wa ardhi na chini yake, "nafaka za kuvunwa" kama vile ngano, shayiri, mahindi, mchele, mtama, na vitu vinginevyo. Katika kuzingatia mambo haya, kuna “kifumbua macho” kutokana na upofu wa ujinga, na “ukumbusho” ambao mtu anakumbushwa kwa huo yale yenye manufaa katika dini na dunia, na mtu anakumbushwa kwa hayo yale ambayo Mwenyezi Mungu alimjulisha na yale waliyosema Mitume wake. Hilo si kwa kila mtu, bali “kwa mja mwenye kurejea (kwa Mwenyezi Mungu)." Yule anayeelekea kwake kwa upendo, hofu, matumaini, na kuitikia mwenye kumuomba. Na ama mwenye kukadhibisha au mwenye kupeana mgongo, basi ishara zote na maonyo hayawafai kitu watu wasioamini. Jumla ya hayo ni kwamba yaliyomo ndani yake ya uumbaji, nguvu, na ugumu ni ushahidi wa ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na yaliyomo ndani yake ya uzuri, ustadi mkubwa, ufundi na uumbaji wa hali ya juu ni ushahidi kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuhukumu vyema zaidi ya mahakimu wote, na kwamba Yeye anajua mno kila kitu, na yale yaliyomo ndani yake ya manufaa na masilahi kwa waja wake ni ushahidi wa rehema ya Mwenyezi Mungu, ambayo imeenea kila kitu, na kupeana kwake kwa wingi ambako kumejumuisha kila kilicho hai. Na viumbe vikuu vilivyomo ndani yake na mpangilio wake wa ajabu ni ushahidi kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mmoja, wa Pekee, Mkusudiwa ambaye hakujifanyia mke wala mwana, wala hana anayelingana naye hata, na kwamba ni Yeye ambaye hakuna kinachostahiki kuabudiwa, kumnyenyekea, kumpenda isipokuwa Yeye tu. Ndiyo maana akasema, "Na tukaifufua kwa maji nchi iliyokuwa imekufa. Kama hivyo ndivyo utakavyokuwa ufufuaji." Na alipowakumbusha Aya hizi za kimbinguni na za kiardhini, akahofisha na adhabu walizopata umma waliotangulia, na kwamba wasiendelee katika hali yao ya kukadhibisha, yakaja yakawapata yale yaliyowapata ndugu zao waliokadhibisha. Akasema: