Al-Maaida
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَكُلُوا۟ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُ حَلَـٰلًا طَيِّبًا ۚ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ٱلَّذِىٓ أَنتُم بِهِۦ مُؤْمِنُونَ ۸۸
{88} Kisha akaamrisha kinyume cha hali ya washirikina ambao wanaharamisha yale aliyohalalisha Mwenyezi Mungu, kwa hivyo akasema; "Na kuleni katika vile alivyowaruzuku Mwenyezi Mungu, vya halali na vizuri." Yaani, kuleni katika riziki yake ambayo aliwaletea kupitia njia alizowarahisishia, vya halali, na siyo vya wizi, wala unyang'anyi, wala yasiyokuwa hayo katika aina za mali ambazo zinachukuliwa bila ya haki. Na pia vinapaswa kuwa vizuri. Nayo, ni ile ambayo haina uchafu ndani yake. Kwa hivyo, hilo likatoa wachafu miongoni mwa hayawani mwitu na vichafu vinginevyo. "Na mcheni Mwenyezi Mungu" katika kutii amri zake na kujiepusha na makatazo yake; "ambaye nyinyi mnamwamini." Kwa maana Imani yenu kwa Mwenyezi Mungu inawasababishia kumcha na kuchunga haki zake. Kwa maana haiwezi kutimia isipokuwa kwa hayo. Aya hii tukufu iliashiria kwamba akimharamishia kilicho halali kwake miongoni mwa vyakula, na kinywaji, na suria, na kijakazi na mfano wa hayo, basi haviwi haramu kwa kuharamisha kwake. Lakini ikiwa atakifanya, basi itamlazimu kutoa kafara ya kiapo chake. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Ewe Nabii! Kwa nini unaharimisha alichokuhalilishia Mwenyezi Mungu?..." hadi mwisho wa Aya. Hata hivyo, kujiharamishia mke kuna kafara ya dhihar. Na inaingia katika Aya hii kwamba haimfailii mtu kujiepusha na vilivyo vizuri na kujiharamishia; bali avile akitafuta msaada wake katika kumtii Mola wake Mlezi.