An-Nisaa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَلِكُلٍّ جَعَلْنَا مَوَٰلِىَ مِمَّا تَرَكَ ٱلْوَٰلِدَانِ وَٱلْأَقْرَبُونَ ۚ وَٱلَّذِينَ عَقَدَتْ أَيْمَـٰنُكُمْ فَـَٔاتُوهُمْ نَصِيبَهُمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ شَهِيدًا ۳۳
{33} Yani, “Na kila mmoja” katika watu “tumemfanyia warithi.” Yani wanamsimamia na anawasimamia kwa kutiana nguvu, na kunusuriana, kusaidiana katika mambo. “Katika yale waliyoyaacha wazazi wawili na jamaa.” Na hili linajumuisha jamaa wote miongoni mwa asili, na matawi, na wengineo waliobaki. Hao ndio warithi miongoni mwa jamaa. Kisha akataja aina nyingine ya warithi, akasema; “Na wale mliofungamana nao kwa viapo.” Yani mlipeana viapo kwa yale mliyofungamana nao ya mikataba ya muungano juu ya kunusuriana, na kusaidiana, na kushirikiana katika mali na mengineyo. Na yote haya ni katika neema za Mwenyezi Mungu juu ya waja wake. Ambapo warithi wanashirikiana kwa kile ambacho baadhi yao peke yao hawakiwezi. Yeye Mtukufu amesema, “wapeni fungu lao;” yani wapeni wasaidizi fungu lao ambalo wanalazimika kulifanya miongoni mwa kushirikiana, na kusaidiana kwa kisichokuwa cha kumuasi Mwenyezi Mungu; na pia wapeni urithi jamaa wa karibu miongoni mwa warithi. “Hakika, Mwenyezi Mungu ni Shahidi juu ya kila kitu.” Yani anakiona kila kitu kwa elimu yake juu ya mambo yote, na kwa kuona kwake harakati za waja wake, na kusikia kwake sauti zao zote.