An-Nisaa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَلَا تَتَمَنَّوْا۟ مَا فَضَّلَ ٱللَّهُ بِهِۦ بَعْضَكُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۚ لِّلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِّمَّا ٱكْتَسَبُوا۟ ۖ وَلِلنِّسَآءِ نَصِيبٌ مِّمَّا ٱكْتَسَبْنَ ۚ وَسْـَٔلُوا۟ ٱللَّهَ مِن فَضْلِهِۦٓ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمًا ۳۲
Mwenyezi Mungu Mtukufu anawakataza Waumini kutamani alichowafadhilishia baadhi yao kuliko wengine wao miongoni mwa yale yanayowezekana na yale yasiyowezekana. Kwa hivyo, wanawake wasitamani sifa maalum za wanaume ambazo aliwaboresha kwazo kuliko wanawake, wala mwenye ufakiri na upungufu (kutamani) hali ya tajiri na mkamilifu kutamani kutupu tu. Kwa sababu, huu ndio wivu wenyewe. Nao ni kutamani kwamba neema ya Mwenyezi Mungu juu ya wengine iwe yako nao iwaondokee. Na kwa sababu inalazimu kutoridhika na majaaliwa ya Mwenyezi Mungu, na kuishia kuwa na uvivu, na kuwa na matarajio batili ambayo hayafungamani na matendo wala kuchuma. Lakini la kusifiwa ni mambo mawili: Kwamba mja anajitahidi kulingana na uwezo wake kwa yale yatakayomnufaisha katika masilahi yake ya kidini na ya kidunia, na amwombe Mwenyezi Mungu Mtukufu katika fadhila zake. Na wala asiitegemee nafsi yake wala kwa yeyote asiyekuwa Mola wake Mlezi. Na kwa sababu ya haya Yeye Mtukufu akasema, “Wanaume wana fungu katika walivyovichuma,” yani katika matendo yao ambayo husababisha matokeo yanayotarajiwa. “Na wanawake wana fungu katika walivyovichuma.” Hivyo basi, kila mmoja wao hayampati yasiyokuwa yale aliyoyachuma na akayachokea. “Na mwombeni Mwenyezi Mungu katika fadhila zake.” Yani katika masilahi yenu yote katika dini na dunia. Na huu ndio ukamilifu wa mja na anuani ya furaha yake. Si yule aliyeacha matendo au aliyeitegemea nafsi yake, asiyemhitaji Mola wake Mlezi au akakusanya mambo mawili haya. Huyu hakika ametupiliwa mbali, mwenye hasara. Na kauli yake, “Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu,” yani humpa yule anayemjua kwamba anastahiki, na anamnyima yule anayemjua kwamba hastahiki.