An-Naml
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَإِنَّهُۥ لَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ ۷۷
{77} Na ikiwa hiki ndicho cheo chake cha utukufu, na kuwa uwazi, na kuondoa kila tofauti, na kutoa uamuzi katika kila shida, basi kinakuwa ndicho neema kubwa zaidi ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, lakini siyo kila mtu anayeikabili neema kwa shukrani, na ndiyo sababu akabainisha kuwa faida Yake, na nuru yake, na mwongozo wake ni maalumu tu kwa waumini. Alisema "Nayo hakika ni uwongofu" kutoka kwa upotovu, ubatili, na mchanganyiko, "na rehema" ambayo kwayo vifua vyao vinalainishwa na mambo yao ya kidini na ya kidunia yananyooka, "kwa Waumini" wanaoiamini na kuisadiki, na kuipokea, na kuielekea kwa kuizingatia, na kuatafakari katika maana zake. Basi hawa kwayo wanapata uongofu kufikia njia iliyonyooka na rehema inayojumuisha furaha, na shindi, na kufaulu.