Al-Baqara
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَـٰٓئِكَةِ ٱسْجُدُوا۟ لِـَٔادَمَ فَسَجَدُوٓا۟ إِلَّآ إِبْلِيسَ أَبَىٰ وَٱسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ ٱلْكَـٰفِرِينَ ۳۴
(34) Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaamrisha wamsujudie Adam; kama ishara ya heshima na kumtukuza; na kumwabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa hivyo, wakatii amri ya Mwenyezi Mungu, na wote wakafanya haraka kusujudu “isipokuwa Iblis, alikataa” kusujudu; na akajivuna juu ya amri ya Mwenyezi Mungu, na juu ya Adam, akasema: “Je, nimsujudie uliyemuumba kwa udongo?” Na huku kukataa kwake na kiburi chake ni kutokana na ukafiri uliomfunika. Hapo, ukadhihirika uadui wake kwa Mwenyezi Mungu na Adam na ukafiri wake na kiburi chake. Na katika aya hizi kuna mazingatio na ishara kama vile kuthibitisha usemi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu; na kwamba hajaacha kuzungumza; anasema chochote anachotaka; na anazungumza kwa chochote anachotaka, na kwamba Yeye ni mwenye elimu na hekima. Pia zina mazingatio kwamba ikiwa hekima ya Mwenyezi Mungu itafichikana kwa mja katika baadhi ya viumbe na maamrisho, basi la wajibu juu yake ni kusalimu amri, na kuishutumu akili yake, na kumkiria Mwenyezi Mungu hekima. Na ndani pia kuna utunzaji wa Mwenyezi Mungu wa mambo ya Malaika, na wema wake kwao; kwa kuwafundisha yale wasiyoyajua, na kuwatanabahisha juu ya yale ambayo hakuwafundisha. Na pia kuna fadhila ya elimu kwa namna mbalimbali: Miongoni mwake ni kwamba Mwenyezi Mungu anawajua Malaika wake; kwa elimu na hekima yake. Na miongoni mwake ni kwamba Mwenyezi Mungu aliwafahamisha ubora wa Adam kwa sababu ya elimu, na kwamba hiyo ndiyo sifa bora zaidi inayokuwa katika mja. Na miongoni mwake ni kwamba Mwenyezi Mungu aliwaamrisha wamsujudie Adam ili kumheshimu ilipobainika fadhila ya elimu yake. Na miongoni mwake ni kwamba katika kuwatahini wengine, ni bora zaidi kuwatahini (kwa kuwauliza maswali kwanza, kabla ya kuwapa jawabu), na akishindwa alichotahiniwa, anaambiwa na yule aliye bora (anayejua), na hivi ni bora zaidi badala ya kumwambia (jibu) mwanzoni. Na miongoni mwake ni kuzingatia hali ya wazazi wawili wa watu na majini, na kubanisha ubora wa Adam na fadhila za Mwenyezi Mungu juu yake, na uadui wa Iblisi kwake; na yasiyokuwa hayo miongoni mwa mazingatio.