پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Maryam
سورهٔ ۱۹

Maryam

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۶۱

جَنَّـٰتِ عَدْنٍ ٱلَّتِى وَعَدَ ٱلرَّحْمَـٰنُ عِبَادَهُۥ بِٱلْغَيْبِ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ وَعْدُهُۥ مَأْتِيًّا ۶۱

{61} Kisha akataja kuwa Pepo aliyowaahidi kuingia si kama Pepo nyinginezo, bali ni "Bustani za milele" zisizokuwa na taabu yoyote, wala kuondoka, wala kutoweka, kwa sababu ya upana wake na wingi wa heri, furaha, na uzuri ulio ndani yake; "ambazo aliwaahidi Rahmani (Mwingi wa Rehema) waja wake katika siri." Alizifungamanisha na jina lake, Mwingi wa rehema, kwa sababu zina rehema na ihsani ambayo jicho halijawahi kuona, wala sikio halijawahi sikia, wala hazijawahi kupita katika moyo wa mwanadamu yeyote. Naye Mtukufu aliziita 'rehema yake,' akasema, "Na ama wale ambao nyuso zao zitakuwa nyeupe, basi watakuwa katika rehema ya Mwenyezi Mungu. Wao humo watadumu." Na pia kuzifungamanisha Pepo hizo na rehema yake kunaonyesha uendelevu wa furaha yake, na kwamba zitabakia maadamu rehema yake itabakia, ambayo ndiyo athari yake na sababu yake. Na waja waliokusudiwa katika Aya hii ni wale waja wanaomfanyia Yeye tu uungu, wale waliomuabudu na wakashikamana na sheria zake, basi uja ukawa ndiyo sifa yao, kama ilivyo katika kauli yake, "Na waja wa Mwingi wa rehema" na mfano wake. Tofauti na waja wake kwa sababu ya kuwamiliki kwake tu. Wale ambao hawakumwabudu. Hawa hata ingawa ni waja kwa sababu ya umola wake juu yao, kwa sababu Yeye ndiye aliyewaumba, akawaruzuku na akawaendesha, lakini hawaingii katika waja wanaomfanyia Yeye tu uungu. Nao huu ni uja anaoufanya mja kwa hiari yake, ambao mwenye kuufanya anasifiwa kwa sababu yake. Si kama uja wao ambao ni wa lazima, ambao hauna sifa yoyote ndani yake. Na kauli yake, "katika ghaibu" inawezekana kuwa inarejelea ahadi ya Mwingi wa rehema. Kwa hivyo, maana yake inakuwa ni kwamba Mwenyezi Mungu aliwaahidi hilo ahadi ya ghaibu ambayo hawakuishuhudia wala kuiona, lakini wakaiamini, na wakaisadiki ghaibu yake, na wakaifanyia bidii ijapokuwa hawakuiona. Basi ingekuwa vipi ikiwa wangeiona? Wangekuwa ni wenye kuitafuta kwa bidii kubwa zaidi, na kuitaka vikubwa sana, na kuifanyia bidii kubwa zaidi. Na maana hii inawasifu kwa sababu ya kuamini kwao ghaibu, ambayo ndiyo imani yenye manufaa. Na inawezekana kwamba inarejelea waja wake. Yaani, wale waliomuabudu katika ghaibu bila ya kumuona. Basi hii ndiyo ibada yao ingawa hawakumuona. Na ikiwa wangemwona, basi wangemwabudu kwa bidii kubwa zaidi, na kurudi kwake kwa wingi, na wangempenda zaidi, na kuwa na hamu kubwa zaidi naye. Pia inawezekana kwamba maana yake ni: Bustani hizi ambazo Mwingi wa rehema aliwaahidi waja wake ni miongoni mwa mambo ambayo maelezo hayawezi kuyafahamu na hakuna yeyote anayeyajua isipokuwa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, ndani ya maana hii kuna kutia hamu juu yake na kuzieleza kwa maelezo mazuri yenye kufurahisha nafsi na kumsisimua aliyetulia ili azitafute, na hili linakuwa kama kauli yake, "Nafsi yoyote haijui waliyofichiwa katika hayo yanayofurahisha macho - ni malipo ya yale waliyokuwa wakiyatenda." Na maana hizi zote ni sahihi na zilithibiti, lakini uwezekano wa kwanza ndio bora zaidi, kwa ushahidi wa kauli yake, "Hakika Yeye ahadi yake hakuna shaka itafika." Kwa maana Yeye havunji ahadi yake, naye ndiye mkweli zaidi wa wanaosema.