Al-Israa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
رَّبُّكُمْ أَعْلَمُ بِمَا فِى نُفُوسِكُمْ ۚ إِن تَكُونُوا۟ صَـٰلِحِينَ فَإِنَّهُۥ كَانَ لِلْأَوَّٰبِينَ غَفُورًا ۲۵
{25} Yaani, Mola wenu Mlezi, Mtukufu anajua yaliyofikichika katika siri zenu za heri na shari, naye haangalii matendo yenu na miili yenu, bali anaangalia nyoyo zenu na yaliyomo ndani yake ya heri na shari. "Ikiwa nyinyi mtakuwa wema" kwa namna kwamba utashi wenu na makusudio yenu zinazungukia kwenye radhi za Mwenyezi Mungu, na hamu yenu ni katika kile kinachowaleta karibu naye, na wala hamna utashi thabiti wa asiyekuwa Mwenyezi Mungu katika mioyo yenu, "basi hakika Yeye ni Mwingi wa kuwaghufiria wanaomrudia sana." Kwa hivyo na anajua yule ambaye Mwenyezi Mungu ameuangalia moyo wake na akajua kwamba hakuna chochote ndani yake isipokuwa kutubia kwake, kumpenda, na kupenda kile kinachomfanya kuwa karibu naye. Basi yeye hata kama wakati mwingine akifanya kile kilicho katika maumbile yake ya kibinadamu, basi Mwenyezi Mungu humsamehe, na humghufiria mambo yaliyomkuta tu na si ada yake wala hayafanyi mara kwa mara.