پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Hud
سورهٔ ۱۱

Hud

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۱۰۹

فَلَا تَكُ فِى مِرْيَةٍ مِّمَّا يَعْبُدُ هَـٰٓؤُلَآءِ ۚ مَا يَعْبُدُونَ إِلَّا كَمَا يَعْبُدُ ءَابَآؤُهُم مِّن قَبْلُ ۚ وَإِنَّا لَمُوَفُّوهُمْ نَصِيبَهُمْ غَيْرَ مَنقُوصٍ ۱۰۹

{109} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwambia Mtume wake Muhammad -rehema na amani za mwenyezi mungu zimshukie: - "Basi usiwe katika shaka juu ya yale wanayoyaabudu hao" washirikina. Yaani, usiwe na shaka na hali yao, na kwamba hilo walifanyalo ni batili. Kwani, hawana ushahidi wowote wa kisheria wala wa kiakili, lakini ushahidi wao na mchanganyiko wao ni kuwa wanaabudu kama walivyoabudu baba zao kabla. Na inavyojulikana ni kuwa, hili si mchanganyiko, achilia mbali kutosha kuwa ushahidi. Kwa sababu, maneno ya wasiokuwa Mitume yanatafutiwa ushahidi wala hayatumiki kama ushahidi, hasa mfano wa hawa watu wapotofu, ambao makosa yao na uharibifu wao ni mwingi katika misingi ya dini. Kwa maana, maneno yao, hata kama watakubaliana juu yake, hayo kwa hakika ni makosa na upotofu "Na hakika Sisi tutawatimilizia fungu lao bila ya kupunguzwa." Yaani, ni lazima litawapata fungu lao waliloandikiwa katika dunia hii, hata kama fungu hilo ni nyingi au ni la kupendeza machoni pako, basi hilo halionyeshi utengenevu wa hali yao. Kwa maana Mwenyezi Mungu humpa dunia yule ambaye Yeye anampenda na asiyempenda, lakini hampi imani na Dini sahihi isipokuwa yule ambaye Yeye anampenda. La msingi ni kwamba asidanganywe na makubaliano ya wapotofu juu ya maneno ya wale waliopotoka miongoni mwa baba zao wa zamani, wala juu ya yale aliyowapa Mwenyezi Mungu na akawapa katika dunia hii.