Yunus
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ قَدْ جَآءَتْكُم مَّوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَشِفَآءٌ لِّمَا فِى ٱلصُّدُورِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ ۵۷
{57} Yeye Mtukufu Anasema akiwahimiza viumbe kukifuata Kitabu hiki kitukufu, kwa kutaja sifa zake nzuri za muhimu sana kwa waja. Akasema, "Enyi watu! Yamekwisha wajia mawaidha kutoka kwa Mola wenu Mlezi;" yaani, yanawaaidhi na yanawaonya juu ya matendo yenye kusababisha ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, yenye kulazimu adhabu yake, na yanawatahadharisha juu yake kwa kubainisha athari zake na madhara yake, "na poza ya yale yaliyo katika vifua." Nayo ni Qur'ani hii Tukufu, ambayo ni poza kwa yale yaliyo katika vifua miongoni mwa maradhi ya matamanio yanayozuia kuifuata sheria. Na maradhi ya shaka yanayotia doa katika elimu ya yakini. Kwani, yale yaliyo ndani yake ya mawaidha, kutia moyo, kuhofisha, ahadi nzuri na ahadi ya adhabu ni katika yale yanayomfanya mja awe na hamu na hofu. Na kukipatikana kutaka ndani yake heri na kuhofu maovu, na mawili hayo yakakuwa, kulingana na yale yanayoyajia kwa kujirudia katika maana za Qur-ani, basi hilo litamfanya mja kutanguliza matakwa ya Mwenyezi Mungu mbele ya matamanio ya nafsi yake; na yanakuwa yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu ndiyo yanayopendwa zaidi kwa mja kuliko matamanio ya nafsi yake. Na vile vile yale yaliyomo miongoni mwa hoja mbalimbali na ushahidi ambazo Mwenyezi Mungu alizieleza kueleza kwa kina zaidi na akazibainisha kubainisha kuzuri zaidi jambo ambalo linaondoa shaka zenye kutoa doa katika haki na unafika kwa hayo viwango vya juu zaidi vya yakini. Na ikiwa moyo utakuwa salama kutokana na maradhi yake, na ukavaa nguo za salama, basi viungo vyote vinaufuata. Kwa kuwa hivyo vinatengenea kwa kutengenea kwake, na vinaharibiwa kwa kuharibika kwake. "Na uwongofu, na rehema kwa Waumini." Na uwongofu ni kuijua haki na kuifanyia kazi. Nayo rehema ni yale yanatopatikana miongoni mwa heri na wema, na malipo ya haraka na ya baadaye kwa wanaoongoka kwayo. Basi uwongofu ndiyo njia bora zaidi, nayo rehema ndiyo malengo na matamanio kamili zaidi, lakini hawezi kulifikia hilo wala haliwi rehema isipokuwa kwa Waumini tu. Na ukipatikana uwongofu, nayo rehema inayotokana nayo ikaingia, yanapatikana mafanikio, na kufaulu, na faida, na furaha na raha.