انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · التوبة
السورة ٩

التوبة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٦

وَإِنْ أَحَدٌ مِّنَ ٱلْمُشْرِكِينَ ٱسْتَجَارَكَ فَأَجِرْهُ حَتَّىٰ يَسْمَعَ كَلَـٰمَ ٱللَّهِ ثُمَّ أَبْلِغْهُ مَأْمَنَهُۥ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْلَمُونَ ٦

{6} Kwa kuwa yale yaliyotangulia kuanzia kauli yake, "Na ikiisha miezi mitukufu, basi waueni washirikina popote muwakutapo, na wachukueni na wazingireni, na wavizieni katika kila njia." Ni amri ya jumla katika hali zote, na kwa watu wote miongoni mwao, Yeye Mtukufu akataja kwamba ikiwa masilahi yatahitaji kuwaleta baadhi yao karibu, basi hilo litaruhusika, bali linakuwa lazima. Kwa hivyo akasema, "Na ikiwa yeyote miongoni mwa washirikina atakuomba ulinzi;" yaani, ikiwa atakuomba ulinzi na umzuie na madhara ili ayasikie maneno ya Mwenyezi Mungu na aiangalie hali ya Uislamu, "basi mpe ulinzi ili apate kusikia maneno ya Mwenyezi Mungu." Kisha kama atasilimu, basi ni hivyo. Na kama sivyo, basi mfikishe katika pahali pake pa amani. Yaani, mahali ambapo anakuwa katika amani. Na sababu katika hilo ni kwamba makafiri ni kaumu wasiojua. Kwa hivyo labda kuendelea kwao kuwa katika kufuru yao hiyo ni kutokana na kutojua kwao ikiwa kutaisha, basi watauchagua Uislamu juu yake. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akamwamuru Mtume wake na umma wake ni wenye kumfuata katika hukumu mbalimbali kwamba wampe ulinzi mwenye kutaka kuyasikiliza maneno ya Mwenyezi Mungu. Na katika hili kuna hoja ya wazi ya dhehebu la Ahlus-Sunnah wal-Jama'ah, wanaosema kwamba Qur-ani ni maneno ya Mwenyezi Mungu ambayo hayakuumba. Kwa sababu Yeye Mtukufu ndiye aliyeyazungumza, na akayafungamanisha naye mwenyewe kufungamanisha kwa sifa kwa kile inachokisifu, na ubatili wa dhehebu la Al-Mu'tazila na wale walioichukua kauli yao kwamba Qur'ani iliumbwa. Na ni ngapi katika ushahidi unaoshuhudia ubatili wa kauli hii. Hapa sipo pahali pa kuyataja hayo!