انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · التوبة
السورة ٩

التوبة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٥

فَإِذَا ٱنسَلَخَ ٱلْأَشْهُرُ ٱلْحُرُمُ فَٱقْتُلُوا۟ ٱلْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ وَخُذُوهُمْ وَٱحْصُرُوهُمْ وَٱقْعُدُوا۟ لَهُمْ كُلَّ مَرْصَدٍ ۚ فَإِن تَابُوا۟ وَأَقَامُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَوُا۟ ٱلزَّكَوٰةَ فَخَلُّوا۟ سَبِيلَهُمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ٥

{5} Yeye Mtukufu anasema: "Na ikiisha miezi mitukufu;" yaani, ambayo ni haramu kupigana na washirikina ndani yake walioingia katika agano na waislamu. Nayo ni ile miezi minne ya kutembea, na kutimiza muda kamili kwa yule ambaye ana kipindi cha zaidi ya hicho, basi dhima juu yao itakuwa imeshajitoa. "Basi waueni washirikina popote muwakutapo" katika pahali popote na wakati wowote. "Na wachukueni" kama mateka "na wazingireni" yaani, wafanyieni ugumu, wala msiwaache wawe na ukunjufu katika nchi ya Mwenyezi Mungu na ardhi yake ambayo Mwenyezi Mungu aliwafanyia waja wake kuwa pahali pa ibada. Kwani hawa hawastahili kukaa hapo, wala hawastahiki inchi moja yake. Kwa sababu ardhi ni ardhi ya Mwenyezi Mungu, na wao ni maadui zake wanaomkataa Yeye na Mitume Wake, wanaopigana, ambao wanataka ardhi isiwe na dini yake, na Mwenyezi Mungu anakataa isipokuwa tu kwamba aitimize nuru yake, hata kama makafiri watachukia. "Na wavizieni katika kila njia;" yaani, kila njia ya kati ya milima na mahali wanapopita, na kuweni macho katika kufanya jihadi dhidi yao, na jitahidini sana muwezavyo katika hilo, na msiache kuendelea kuwa katika jambo hili mpaka watubu kutoka katika shirki yao. Na ndiyo sababu akasema: "Lakini wakitubu" kutoka katika ushirikina wao, "na wakasimamisha sala;" yaani, wakaitekeleza kwa haki zake, "na wakatoa Zaka" wakawapa wanaoistahiki; "waachilie njia yao;" yaani waacheni, na ili wawe mfano wenu, wana kile mlicho nacho, na ni juu yao kile kilicho juu yenu. "Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusitiri dhambi, Mwenye kurehemu." Anaisitiri dhambi ya shirki na kilicho chini yake kwa wenye kutubia, na anawarehemu kwa kuwawezesha kutubia, kisha kuikubali kutoka kwao. Na katika Aya hii Kuna ushahidi kwamba yeyote anayekataa kusali au kutoa zaka, basi atapigwa mpaka aitekeleze, kama alivyotumia hilo Abu Bakr as-Siddiq Mwenyezi Mungu amridhie kama ushahidi.