التوبة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيُضِلَّ قَوْمًۢا بَعْدَ إِذْ هَدَىٰهُمْ حَتَّىٰ يُبَيِّنَ لَهُم مَّا يَتَّقُونَ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمٌ ١١٥
{115} Yaani, ikiwa Yeye Mtukufu atawaneemesha kaumu uwongofu na akawaamrisha wafuate njia iliyonyooka, basi Yeye Mtukufu hukamilisha ihsani yake juu yao, na huwabainishia yote wanayohitaji na ni ya dharura sana kwao. Na hawaachi kupotea na kutojua mambo ya dini yao. Basi katika hili kuna ushahidi wa ukamilifu wa rehema yake, na kwamba sheria yake inatosha kila wanachokihitaji waja wake katika misingi ya dini na matawi yake. Na inawezekana kwamba maana yake ni kuwa "Na haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwapotosha kaumu baada ya kwisha waongoa mpaka awabainishie ya kujiepusha nayo.” Basi anapowabainishia yale wanayopaswa kujiepusha nayo, lakini wasiyafuate, anawaadhibu kwa upotofu kama malipo ya kukataa kwao haki iliyo wazi, lakini ile maana ya kwanza ni bora zaidi. "Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema kila kitu.” Basi kwa sababu ya ukamilifu wa elimu yake na ujumla wake, aliwafundisha ambayo hamkuwa mnayajua, na akawabainishia yale mtakayofaidika nayo.