التوبة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
إِنَّ ٱللَّهَ لَهُۥ مُلْكُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۖ يُحْىِۦ وَيُمِيتُ ۚ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِن وَلِىٍّ وَلَا نَصِيرٍ ١١٦
{116} "Hakika Mwenyezi Mungu anao ufalme wa mbingu zote na ardhi; huhuisha na hufisha.” Yaani, Yeye ndiye Mmiliki wa hayo, Mwenye kuwaendesha waja wake kwa kuwahuisha na kuwafisha, na aina mbalimbali za uendeshaji mambo ya kiungu. Kwa hivyo ikiwa hatii dosari katika kuendesha mambo kwake kwa kimajaliwa, basi vipi atatia dosari katika kuenda mambo kwake kwa kidini, kunakohusiana na uungu wake, na akawaacha waja wake bure na wakiwa wamepuuzwa, au awaache wapotee, huku hawajui chochote, na hali Yeye ndiye mkuu zaidi wa kuwasimamia waja wake? Na ndiyo maana akasema: "Nanyi hamna mlinzi yeyote wala msaidizi kando na Mwenyezi Mungu.” Yaani, mlinzi atakayewasimamia kwa kuwaletea manufaa au mwenye kuwanusuru atakayewazuia kutokana na madhara.