الأنعام
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قُل لَّآ أَجِدُ فِى مَآ أُوحِىَ إِلَىَّ مُحَرَّمًا عَلَىٰ طَاعِمٍ يَطْعَمُهُۥٓ إِلَّآ أَن يَكُونَ مَيْتَةً أَوْ دَمًا مَّسْفُوحًا أَوْ لَحْمَ خِنزِيرٍ فَإِنَّهُۥ رِجْسٌ أَوْ فِسْقًا أُهِلَّ لِغَيْرِ ٱللَّهِ بِهِۦ ۚ فَمَنِ ٱضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَإِنَّ رَبَّكَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ١٤٥
{145} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kuwashutumu washirikina kwa yale waliyoyaharamisha ya halali na wakayanasibisha kwa Mwenyezi Mungu, na akaibatilisha kauli yao hiyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akamwaamrisha Mtume wake kwamba awabainishie watu yale ambayo Mwenyezi Mungu amewaharamishia; ili wajue kuwa chochote kisichokuwa hayo ni halali; na mwenye kunasibisha kuharamishwa kwake kwa Mwenyezi Mungu, ni mwongo mwenye batili. Kwa sababu, kuharamisha hakutoki isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu juu ya ulimi wa Mtume wake, na tayari alikwisha mwambia Mtume wake: "Sema: Sipati katika yale niliyofunuliwa mimi kitu kilichoharamishwa kwa mlaji." Yaani, kilichoharamishwa kukila bila ya kuangalia uharamu wa kunufaika kwa kutokila na kutofanya hivyo, "isipokuwa ikiwa ni nyamafu." Na nyamafu ni yule aliyekufa bila kuchinjwa kisheria, kwa sababu huyo si halali. Kama yeye Mtukufu alivyosema: "Mmeharimishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe," "au damu inayomwagika." Nayo ni damu inayotoka katika mnyama aliyechinjwa anapochinjwa kisheria. Na hiyo ni damu ambayo inadhuru kuizuilia katika mwili. Na inapotoka nje ya mwili, basi madhara ya kuila nyama hiyo yanaondoka. Na maana isiyokuwa ya moja kwa moja ya aya hii ni kuwa damu inayobakia katika nyama na mishipa baada ya kuchinja ni halali na safi, "au nyama ya nguruwe, kwani huo ni uchafu;" yaani, vitu hivi vitatu ni uchafu, vyenye kudhuru, ambavyo Mwenyezi Mungu aliwaharamishia hivyo kwa sababu ya kuwafanyia upole kuwasafisha kutokana na kukaribia vichafu. "Au" isipokuwa ikiwa ni "kilichovukiwa mipaka katika kilichochinjwa kwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu." Yaani, isipokuwa ikiwa mnyama huyo aliyechinjwa alichinjwa kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu, miongoni mwa viabudiwa vyote na miungu ambao wanaiabudu washirikina. Basi hivi ni katika Fusuuq, ambayo ni kutoka katika utii kwa Mwenyezi Mungu hadi kwenye kumuasi. Na pamoja na haya, vitu hivi viliharamishwa, mwenye kulazimishwa kuvitumia. Yaani, haja na ulazima vilimpelekea kula kitu katika hivyo kama hakuwa na kitu, na akahofia nafsi yake kuharibika, "bila ya kutamani wala kupita mipaka." Na maana ya "bila ya kutamani" ni bila ya kutaka kukila bila ya kuwepo dharura, wala kuvuka mipaka, yaani kuvuka kikomo, kwa kula zaidi ya haja yake. "Lakini mwenye kushikwa na dharura, bila ya kutamani wala kupita mipaka, basi hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu." Yaani, Mwenyezi Mungu amemsamehe yule aliyekuwa katika hali hii. Na Wanachuoni, Mwenyezi Mungu awarehemu, wamehitalifiana kuhusu kufungia huku kulikotajwa katika Aya hii, pamoja na kwamba kuna vilivyoharamishwa ambavyo havikutajwa ndani yake. Kama vile wanyama wa porini wanaowinda, na kila ndege mwenye kucha za kuwindia na mfano wa hao. Basi baadhi yao walisema: Hakika Aya hii iliteremka kabla ya kuharamishwa kwa yale yaliyo zaidi ya yale yaliyotajwa ndani yake. Kwa hivyo, kufungia huku kulikotajwa ndani yake hakupingani na uharamu uliokuja baadaye baada ya hapo. Kwa sababu hakukupata katika yale yaliyoteremshwa kwake wakati huo. Na baadhi yao walisema: Hakika Aya hii inajumuisha vitu vyote vilivyoharamishwa, ambavyo baadhi yake viko waziwazi, na baadhi yake vinachukuliwa kutoka katika maana yake isiyokuwa ya moja kwa moja na kutoka katika ujumla wa sababu. Kwa maana Kauli yake yeye Mtukufu katika kubainisha sababu ya maiti, na damu, na nyama ya nguruwe, au ya mwisho yake tu "kwani huo ni uchafu" ni maelezo yanayojumuisha kila kilichoharamishwa. Kwa sababu yale yote yaliyoharamishwa ni machafu na mabaya, nayo ni miongoni mwa mambo mabaya na machafu ambayo Mwenyezi Mungu amewaharamishia waja wake ili kuwalinda na kuwatukuza ili wasiguse mabaya na machafu. Na yanachukuliwa maelezo ya kina ya uchafu ulioharamishwa kutoka katika Sunnah. Kwa maana hiyo inaifafanua Qur-aani na inaeleza makusudio yake. Kwa hivyo ikiwa Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuharamisha katika vyakula isipokuwa yale yaliyotajwa, na kuharamisha chanzo chake hakiwi isipokuwa sheria ya Mwenyezi Mungu. Hilo linaashiria kuwa washirikina ambao waliharamisha yale aliyowaruzuku Mwenyezi Mungu wanamzulia Mwenyezi Mungu uongo, wanasema kumhusu kwa yale ambayo hakuyasema. Na katika aya hii Kuna uwezekano mkubwa, lau Mwenyezi Mungu asingemtaja nguruwe ndani yake. Nao ni kuwa muktadha ni katika kukanusha kauli za washirikina zilizotangulia kuhusu kuharamisha kwao yale aliyohalalisha Mwenyezi Mungu na kuingia kwao katika hilo kulingana na yale ambayo nafsi zao zinawaambia; na hayo ni katika mifugo hasa. Na hakuna kilichoharamishwa katika hao isipokuwa wale waliotajwa katika aya hii, nyamafu wake na wale waliochinjwa kwa ajili ya asiyekuwa mwenyezi Mungu, na wasiokuwa hao, basi hao ni halali. Na pengine sababu ya kumtaja nguruwe hapa kwa uwezekano huu ni kwamba baadhi ya watu wasiojua wanaweza kumuingiza katika mifugo, na kwamba yeye ni aina katika aina za kondoo. Kama walivyofikiri hivyo wajinga katika Wakristo na mfano wao, wakawa wanamkuza kama wanavyowakuza mifugo, na hawatofautishi baina yake na mifugo walio halali.