انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الأنعام
السورة ٦

الأنعام

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٤٦

وَعَلَى ٱلَّذِينَ هَادُوا۟ حَرَّمْنَا كُلَّ ذِى ظُفُرٍ ۖ وَمِنَ ٱلْبَقَرِ وَٱلْغَنَمِ حَرَّمْنَا عَلَيْهِمْ شُحُومَهُمَآ إِلَّا مَا حَمَلَتْ ظُهُورُهُمَآ أَوِ ٱلْحَوَايَآ أَوْ مَا ٱخْتَلَطَ بِعَظْمٍ ۚ ذَٰلِكَ جَزَيْنَـٰهُم بِبَغْيِهِمْ ۖ وَإِنَّا لَصَـٰدِقُونَ ١٤٦

{146} Basi haya yaliyoharimishwa kwa Ummah huu yote ni kwa njia ya kuwasafisha na kuwalinda. Na ama yale aliyowaharamishia Watu wa Kitabu, baadhi yake ni mazuri, lakini yaliharamishwa kwao kuwa ni adhabu kwao. Na ndiyo maana akasema, "Na wale waliotubu (yani Mayahudi) tuliwaharimishia kila mwenye kwato au mguu usio na mgawanyiko." Na hao ni kama vile ngamia na mfano wake. Na tuliwaharimishia baadhi ya sehemu za ng'ombe na kondoo, ambayo ni shahamu yao. Lakini kilichoharamishwa si shahamu yao yote, bali ni shahamu ya kwenye makalio na ile inayofunika rumeni na matumbo, na kwa sababu hiyo akatoa katika hilo shahamu iliyo halali. Akasema, "isipokuwa ile iliyobeba migongo yao au matumbo yao." Yaani, shahamu iliyochanganyika na matumbo, "au iliyochanganyika na mifupa. Hayo" maharamisho kwa Mayahudi - "tuliwalipa kwa sababu ya uasi wao." Yaani, dhuluma yao na kuvuka kwao mipaka katika haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akawaharimishia vitu hivi kuwa ni mateso na adhabu kwao. "Nasi bila ya shaka ni wakweli" katika kila tunalolisema, na tunalolifanya, na tunalolihukumu kwalo. Na ni nani mkweli zaidi katika usemi kuliko Mwenyezi Mungu? Na ni nani mzuri zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa kaumu wenye yakini?