المائدة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
مَا جَعَلَ ٱللَّهُ مِنۢ بَحِيرَةٍ وَلَا سَآئِبَةٍ وَلَا وَصِيلَةٍ وَلَا حَامٍ ۙ وَلَـٰكِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ يَفْتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلْكَذِبَ ۖ وَأَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ ١٠٣
{103} Huku ni kwashutumu washirikina ambao walitunga sheria katika dini yake ambayo Mwenyezi Mungu hakuidhinisha, na wakaviharamisha vile alivyovihalalisha Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, kwa maoni yao mabovu wakawafanya baadhi ya mifugo wao kuwa haramu kulingana na makubaliano yao, ambayo yanapingana na yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo Akasema; "Mwenyezi Mungu hakuweka uharamu wowote juu ya 'Bahira,'" naye ni ngamia wa kike wanayemtoboa sikio lake, kisha wanaharamisha kumpanda, na wanamuona kuwa ni wa heshima. "Wala "Saiba," naye ni ngamia wa kike, au ng'ombe wa kike, au kondoo anapokifikia kitu walichokubaliana juu yake, wanamwachilia huru, basi hapandwi, wala haibebwi juu yake, wala haliwi; na baadhi yao waliwekwa nadhiri katika mali yake ili aachiliwe huru. "Wala "Hami;" yaani, ngamia ambaye mgongo wake umekingwa dhidi ya kupandwa wala kubebeshwa anapofika katika hali inayojulikana baina yao. Na yote hayo ni katika yale ambayo washirikina waliyaharamisha bila ya ushahidi wala hoja. Bali huku ni kumzulia Mwenyezi Mungu kunatokana na ujinga wao na kutokuwa na akili kwao. Na ndiyo maana akasema, "Lakini wale waliokufuru ndio humzulia uongo Mwenyezi Mungu, na wengi wao hawatumii akili." Kwa hivyo, hayo hayana upokezi wa hoja ya kimaandiko, wala hoja ya kiakili.