انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · المائدة
السورة ٥

المائدة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٠٤

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا۟ إِلَىٰ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ وَإِلَى ٱلرَّسُولِ قَالُوا۟ حَسْبُنَا مَا وَجَدْنَا عَلَيْهِ ءَابَآءَنَآ ۚ أَوَلَوْ كَانَ ءَابَآؤُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ شَيْـًٔا وَلَا يَهْتَدُونَ ١٠٤

{104} Na pamoja na haya, wao hakika walivutiwa na maoni yao, ambayo yalijengwa juu ya ujinga na udhalimu. Basi wakiitwa "kwenye yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, na kwa Mtume;" wanapeana mgongo na hawakubali na hugeuka na wala hawakubali, na "wanasema: Yanatutosha tuliyowakuta nayo baba zetu;" katika Dini, hata kama si ya sawasawa, wala dini yenye kuwaokoa na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na kama baba zao wangekuwa na utoshelevu, na maarifa na kujua, basi jambo hili lingekuwa rahisi; lakini baba zao hawaelewi chochote. Yaani, hawana lolote katika yale yanayoeleweka, wala chochote katika elimu na uwongofu. Basi na angamie yule ambaye anajifananisha na yule asiyekuwa na elimu sahihi wala akili nzuri, na akaacha kufuata yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu; na kuwafuata Mitume wake, ambao wanazijaza nyoyo elimu, na imani, na uongofu na yakini.