انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · البقرة
السورة ٢

البقرة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٠٦

مَا نَنسَخْ مِنْ ءَايَةٍ أَوْ نُنسِهَا نَأْتِ بِخَيْرٍ مِّنْهَآ أَوْ مِثْلِهَآ ۗ أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ ١٠٦

(106) (An-Naskh) Ufutaji ni uhamisho. Na uhakika wa ufutaji ni kuwahamisha Mukallafin (yani anayewajibika kutekeleza sheria) kutoka hukumu ya kisheria moja kwenda kwa hukumu nyingine, au kuifutilia mbali. Na Mayahudi walikuwa wakiukanusha ufutaji na kudai kuwa hauruhusiki. Nao (ufutaji) umetajwa kwao katika Taurati. Kwa hivyo, kuukanusha kwao ni kufuru na matamanio matupu. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akafahamisha kuhusu hekima yake katika ufutaji, na kwamba hafuti "ishara (aya) au tunayoisahaulisha" yani tunawasahaulisha waja, na tunaiondoa kutoka kwa nyoyo zao "tunaileta iliyo bora kuliko hiyo" na yenye manufaa zaidi kwenu; "au iliyo mfano wake." Basi ikaashiria kuwa ufutaji hauwi kwa lenye manufaa kidogo kwenu kuliko (ishara) ya kwanza. Kwa sababu, fadhila zake Mwenyezi Mungu Mtukufu huongezeka, hasa juu ya umma huu ambao amewarahisishia mno dini yao. Na akasema kwamba mwenye kuukashifu ufutaji [basi kwa hakika] ameukashifu ufalme wake na uwezo wake. Akasema :"Je, hujui kwamba Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu?"