انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الإسراء
السورة ١٧

الإسراء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ٢٦–٢٧

وَءَاتِ ذَا ٱلْقُرْبَىٰ حَقَّهُۥ وَٱلْمِسْكِينَ وَٱبْنَ ٱلسَّبِيلِ وَلَا تُبَذِّرْ تَبْذِيرًا ٢٦ إِنَّ ٱلْمُبَذِّرِينَ كَانُوٓا۟ إِخْوَٰنَ ٱلشَّيَـٰطِينِ ۖ وَكَانَ ٱلشَّيْطَـٰنُ لِرَبِّهِۦ كَفُورًا ٢٧

{26-27} Yeye Mtukufu anasema, "Na mpe aliye jamaa yako haki yake" kama vile kumfanyia wema, na kumkirimu kwa wajibu na kusiko kwa wajibu. Na haki hizo zinatofautiana kulingana na hali tofauti tofauti, jamaa, mahitaji, na kutohitaji, na nyakati. "Na maskini" mpe haki yake katika mali ya zakat yake na mali nynginezo, ili umaskini wake uishe. "Na msafiri aliyekatikiwa" ambaye hayukao katika mji wake. Kwa hivyo wote watapewa katika maili hiyo kwa njia ambayo haimdhuru mtoaji, na wala isiyozidi kiasi kinachofaa. Kwa maana, hilo kutumia ovyo kwa fujo ambako Mwenyezi Mungu alikataza na akasema kwamba hakika watumiao ovyo kwa fujo, "ni ndugu wa mashetani." Kwa sababu Shetani analingania katika sifa inayokashifiwa. Basi yeye humuita mtu katika ubahili na kushikilia mali bila ya kuitoa. Kwa hivyo, anapomuasi, anamuita katika kupitiliza kiasi na kutoa ovyo kwa fujo. Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu anaamrisha kutenda mambo yenye uadilifu mkubwa zaidi na ya haki zaidi, na anasifu juu yake, kama ilivyo katika kauli yake kuhusu waja wa Mwingi wa rehema walio wema. "Na wale ambao wanapotoa mali zao, hawatoi kwa kupitiliza kiasi wala hawafanyi ubahili, bali wanasimama sawasawa katikati baina ya hayo."