Al-Maaida
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ ٱلنَّاسِ عَدَٰوَةً لِّلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱلْيَهُودَ وَٱلَّذِينَ أَشْرَكُوا۟ ۖ وَلَتَجِدَنَّ أَقْرَبَهُم مَّوَدَّةً لِّلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱلَّذِينَ قَالُوٓا۟ إِنَّا نَصَـٰرَىٰ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّ مِنْهُمْ قِسِّيسِينَ وَرُهْبَانًا وَأَنَّهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ 82
{82} Yeye Mtukufu anasema katika kubainisha kundi lililo karibu zaidi na Waislamu kati ya makundi haya mawili, na lililo karibu katika kuwafanya kuwa marafiki, na kuwapenda, na wale wao walio mbali zaidi na hayo. “Hakika utawakuta walio na uadui mkubwa mno kuliko watu wote juu ya wale walioamini ni Mayahudi na wale walioshirikisha.” Madhehebu haya mawili makubwa ndiyo wenye uadui mkubwa kabisa katika watu wote dhidi ya Uislamu na Waislamu, na ndiyo yenye juhudi kubwa zaidi kati yao katika kuwafikishia madhara. Na hilo ni kwa sababu ya chuki yao kubwa kwao, na dhuluma, na husuda, na ukaidi, na ukafiri. "Na hakika utawakuta wale wao walio karibu mno kwa mapenzi kwa wale walioamini ni wale waliosema: Hakika Sisi ni Manasara." Na Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja sababu kadhaa za hilo: Miongoni mwake ni kwamba, miongoni mwao wamo “makasisi na wamonaki.” Yaani, wanachuoni walioipa dunia mgongo, na waja wafanyao ibada kwa wingi katika nyumba za watawa. Na kuwa na elimu pamoja na kuipa dunia mgongo, na vile vile ibada ni katika yenye kuupa moyo upole, na kuulainisha, na huuondolea yale yaliyomo ya usugu na ugumu. Na ndiyo maana ugumu wa Mayahudi na ukali wa washirikina haupatikani ndani yao. Miongoni mwake ni "kwamba wao hawafanyi kiburi;" yaani, hawana kiburi wala jeuri ndani yao katika kuifuata haki. Na hilo linasababisha kuwa kwao karibu na Waislamu, na kuwapenda. Kwa maana, Mnyenyekevu yuko karibu zaidi na heri kuliko mwenye kiburi.