Al-Maaida
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ كُونُوا۟ قَوَّٰمِينَ لِلَّهِ شُهَدَآءَ بِٱلْقِسْطِ ۖ وَلَا يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَـَٔانُ قَوْمٍ عَلَىٰٓ أَلَّا تَعْدِلُوا۟ ۚ ٱعْدِلُوا۟ هُوَ أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ ۖ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ خَبِيرٌۢ بِمَا تَعْمَلُونَ 8
{8.} Yaani, "Enyi mlioamini!" katika yale waliyoamrishwa kuyaamini, shikamaneni na yale yanayoambatana na imani yenu, kwamba muwe "wasimamao madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wenye kushuhudia kwa haki." Kwa kuwa mkakamavu katika kuisimamia haki kwa harakati zenu za nje na za ndani, kwamba kusimama huko kuwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu pekee na si kwa ajili ya lengo lolote miongoni mwa malengo ya kidunia. Na kwamba muwe mnakusudia haki, ambayo ni uadilifu, siyo kupita kiasi wala kupunguza kiasi katika maneno yenu au vitendo vyenu, na mumfanyie hivyo wa karibu na wa mbali, rafiki na adui. "Na Wala kamwe kusiwapelekee," yani kuwachukia watu kusiwafanye "kutofanya uadilifu," kama afanyavyo yule asiyekuwa na uadilifu wala haki, bali kama mnavyomshuhudia rafiki yenu. Basi shuhudieni dhidi yake, kama mnavyoshuhudia dhidi ya adui yenu, basi kuweni mashahidi wake hata akiwa ni kafiri au mzushi. Kwa maana ni lazima kumfanyia uadilifu na kukubali haki anayokuja nayo. [Kwa sababu ni haki], si kwa sababu aliisema, na wala haki haikataliwi kwa sababu ya kuisema, kwani hii ni dhaluma. "Fanyeni uadilifu. Hivyo ndiyo kuwa karibu mno na uchamungu." Yaani, kila mnavyoifanyia hima haki na mkajitahidi kuifanyia kazi, hilo linakuwa karibu zaidi na uchamungu wa mioyo yenu. Na uadilifu ukitimia, uchamungu unakamilika. "Hakika Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda," na atawalipa kwa matendo yenu, mema yake na mabaya yake, madogo yake na makubwa yake, malipo ya sasa na ya baadaye.