An-Nisaa
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
وَلَأُضِلَّنَّهُمْ وَلَأُمَنِّيَنَّهُمْ وَلَـَٔامُرَنَّهُمْ فَلَيُبَتِّكُنَّ ءَاذَانَ ٱلْأَنْعَـٰمِ وَلَـَٔامُرَنَّهُمْ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلْقَ ٱللَّهِ ۚ وَمَن يَتَّخِذِ ٱلشَّيْطَـٰنَ وَلِيًّا مِّن دُونِ ٱللَّهِ فَقَدْ خَسِرَ خُسْرَانًا مُّبِينًا 119
{119} Na hili fungu maalumu ambalo alimuapia Mwenyezi Mungu kwamba atawachukua, alitaja yale anayowatakia, na anacholenga kutoka kwao kwa kauli yake. "Na hakika nitawapoteza," yani, kutoka katika njia iliyonyooka. Upotevu katika elimu na upotovu katika vitendo, "na nitawatia matumaini ya uongo." Yani, pamoja na kuwapotoa nitawatia matumaini ya uongo kwamba watayafikia yale waliyoyapata waongofu. Na huku ndiko kuhadaa kwenyewe. Kwani haukuishia katika kuwapoteza tu, mpaka akawapambia yale waliyo ndani yake ya upotovu, na huku ni kuzidishiwa uovu juu ya uovu wao. Kwa kuwa walifanya vitendo vya watu wa Motoni vyenye kusababisha adhabu, na wakadhani kuwa hayo yanasababisha kuingia katika Pepo. Basi Fikiria hilo kuhusu Wayahudi, na Wakristo, na kadhalika. Kwani wao kama alivyosimulia Mwenyezi Mungu juu yao, "Na walisema: Hataingia Peponi ila aliyekuwa Yahudi au Mkristo. Hayo ni matumaini yao ya uongo." "Na namna hivyo tumewapambia kila umma vitendo vyao." "Sema: Je, tuwaambie wenye hasara mno katika vitendo vyao? Ni wale ambao juhudi yao katika maisha ya dunia ilipotea bure, nao wakadhani kwamba wanafanya matendo mazuri..." hadi mwisho wa Aya. na Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema kuhusu wanafiki kuwa Watawambia Waumini Siku ya Kiyama: "Je hatukuwa pamoja nanyi? Watawaambia: Ndiyo, lakini mlijifitini wenyewe, na mkasitasita, na mkatia shaka, na matumaini ya uongo ya nafsi zenu yakawadanganya, mpaka ikaja amri ya Mwenyezi Mungu, na yule mdanganyifu akawadanganya msimfuate Mwenyezi Mungu." Na kauli yake, "na nitawaamrisha, basi watakata masikio ya wanyama." Na hilo ni kama vile Al-Bahiira, na As-Saibah, na Al-Wasila, na Al-Haam. Basi akatanabahisha kwa baadhi ya hayo juu ya mengineyo yote. Na hii ni aina ya upotofu inayolazimu kuharamisha kile ambacho Mwenyezi Mungu alihalalisha, au kuhalalisha kile ambacho Mwenyezi Mungu ameharamisha. Na zinaambatana na hayo itikadi potofu na hukumu za dhuluma, ambazo ni miongoni mwa upotofu mkubwa zaidi. "Na nitawaamrisha, basi watabadili aliyoumba Mwenyezi Mungu." Na hili linachukua [kubadilisha] umbile la dhahiri kwa kujichora chake, na kuchonga nywele za usoni, na kuweka nafasi kati ya meno kwa sababu ya kujirembesha, na mambo mengine aliyowadanganya nayo Shetani, kwa hivyo wakabadilisha umbile la Mwingi wa Rehema. Na hilo linajumuisha kutoridhika na kuumba kwake, na kutia dosari katika hekima yake. Na kuamini kwamba kile wanachokifanya kwa mikono yao ndicho bora zaidi kuliko kuumba kwa Mwingi wa Rehema, na kutoridhika na majaaliwa yake na uendeshaji mambo wake. Na pia inachukua kubadilisha tabia ya ndani, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaumba waja wake wakiwa wanyoofu wakiwa katika umbile la asili la kukubali haki na kuipendelea. Kisha mashetani wakawajia, na wakawang’oa katika uumbaji huu mzuri, na wakawapambia uovu, na ushirikina, na ukafiri, kutoka nje ya mipaka, na maasia. Kwa maana, kila mtoto anazaliwa kwenye umbile la asili, kisha wazazi wake wanamfanya kuwa Myahudi, au Mkristo, au Majusi, na mfano wa hayo. Miongoni mwa yale ambayo kwayo wanabadilisha kile ambacho Mungu amewaumba juu yake waja Wake miongoni mwa kumpwekesha Yeye, na kumpenda, na kumjua. Lakini mashetani wakawawinda katika mahali hapa kama kuwinda kwa mnyama mwitu na mbwa-mwitu kwa kondoo aliye peke yake. Lau kuwa si upole wa Mwenyezi Mungu na ukarimu wake kwa waja Wake wampwekeshaye Yeye, basi yangewatokea yale yaliyowatokea hawa waliofitinishwa. Na haya yaliyowapata ya kumfanya rafiki adui wao anayewatakia maovu kwa namna zote, na wakahasiri dunia na akhera, na wakarudi wameambulia patupu na mapatano yenye hasara. Na ndiyo maana akasema, "Na mwenye kumfanya Shetani kuwa ni rafiki mwandani badala ya Mwenyezi Mungu, basi hakika amehasiri hasara ya dhahiri." Na ni hasara gani iliyo dhahiri zaidi na kubwa zaidi kuliko yule aliyepoteza dini yake na dunia yake, na maasia yake na makosa yake yakamwangamiza, na akapata taabu ya milele, na akakosa neema ya milele? Vivyo hivyo, mwenye kumfanya rafiki bwana wake na akapendelea ridhaa yake, atapata faida yote, na atafaulu kufaulu kwote, na atapata furaha katika Nyumba zote mbili, na atakuwa mwenye utulivu machoni pake. Na Hakuna wa kuzuia kile Ulichopeana, wala hakuna mwenye kupeana kile ulichokizuia. Ewe Mwenyezi Mungu! Tufanye marafiki miongoni mwa wale uliowafanya kuwa marafiki wako, na utupe salama miongoni mwa wale uliowapa salama.