İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Noor
Sure 24

An-Noor

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

Ayet 4

وَٱلَّذِينَ يَرْمُونَ ٱلْمُحْصَنَـٰتِ ثُمَّ لَمْ يَأْتُوا۟ بِأَرْبَعَةِ شُهَدَآءَ فَٱجْلِدُوهُمْ ثَمَـٰنِينَ جَلْدَةً وَلَا تَقْبَلُوا۟ لَهُمْ شَهَـٰدَةً أَبَدًا ۚ وَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْفَـٰسِقُونَ 4

{4} Alipolifanya kubwa Mwenyezi Mungu Mtukufu jambo la zinaa, kwa kuwajibisha kutandikwa kwake viboko mia moja na kupigwa mawe ikiwa ameoa, na kwamba haijuzu kushirikiana naye au kujichanganya naye kwa namna ambayo mja hatasalimika ndani yake na shari. Amebainisha Mwenyezi Mungu Mtukufu ukubwa wa kutanguliza hadhi na heshima kwa masingizio ya uzinifu. Akasema, "Na wanaowasingizia wanawake mahashumu." Yaani, wanawake walio huru na waadilifu wenye kujiheshimu na vilevile wanaume, hakuna tofauti baina ya mambo mawili, na kinachomaanishwa na kusingiziwa ni kusingiziwa kwa uzinzi; kwa ushahidi wa muktadha. "Kisha wasilete," kwa sababu yale waliomsingizia, "mashahidi wanne." Yaani, watu waadilifu watakaoshuhudilia kwa hilo waziwazi. "Basi watandikeni bakora themanini," kwa mjeledi wa wastani unaoumiza, na wala asizidishe kwa hilo kupita kiasi mpaka ikamfisidi; kwa sababu malengo ni kuadibu, si kuangamiza. Katika hii, kuna kuamuliwa kwa adhabu ya kashfa, lakini kwa sharti awe mtu anayesingiziwa kama alivyosema Mwenyezi Mungu aliyetukuka, mtu aliye ndani ya ndoa na mwaminifu. Ama kumkashifu mtu ambaye si aliye kwenye ndoa; inahitaji adhabu ya taazir kama vile kumpa ushauri na nasaha. "Na msiwakubalie ushahidi wao tena." Yaani, wana adhabu nyengine, nayo ni kuwa ushahidi wa mwenye kusingizia haukubaliki, hata akiadhibiwa kwa kashfa, mpaka atubie; kama inavyofuata. "Na hao ndio wapotovu." Yaani, wale wanaokengeuka katika kumtii Mwenyezi Mungu, ambao shari na uovu wao umeongezeka, na hiyo ni kwa sababu ya kukiuka alichoharamisha Mwenyezi Mungu, na kumvunjia heshima ndugu yake, na kuwalazimisha watu kuyazungumza aliyoyasema, na kuondoa udugu aliouweka Mwenyezi Mungu miongoni mwa watu wa imani, na kupenda uenee uchafu miongoni mwa walioamini. Na huu ni ushahidi kwamba kashfa ni dhambi kubwa.