İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Hajj
Sure 22

Al-Hajj

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

Ayet 27

وَأَذِّن فِى ٱلنَّاسِ بِٱلْحَجِّ يَأْتُوكَ رِجَالًا وَعَلَىٰ كُلِّ ضَامِرٍ يَأْتِينَ مِن كُلِّ فَجٍّ عَمِيقٍ 27

{27} "Na watangazie watu Hija;" yaani, wafundishe juu yake, na waite kwayo, na wajulishe walio karibu nao na walio mbali nao juu ya faradhi na wema wake. Kwa hivyo ukiwaalika; watakujia kama mahujaji (wa Hijja) na mahujaji (wa umra) "kwa miguu." Yaani, wenye kutembea kwa miguu yao kwa kutamani, "na juu ya kila ngamia aliyekonda." Yaani ngamia aliyekonda anayemaliza kazi na misheni, na anaendelea na safari yake mpaka akafika mahali pazuri kabisa. "Wakija kutoka katika kila njia ya mbali;" yaani, kutoka kila nchi ya mbali. Al-Khalil, amani iwe juu yake, akafanya hivyo, na baada yake mwanawe Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimfikie, - wakawaita watu wahiji katika Nyumba hii, wakaendelea na kuirudia, na kile ambacho Mwenyezi Mungu aliahidi kilitimia. Watu wakamjia, wanaume na wanawake, kutoka mashariki na magharibi ya ardhi.