İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sure 2

Al-Baqara

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

Ayet 194

ٱلشَّهْرُ ٱلْحَرَامُ بِٱلشَّهْرِ ٱلْحَرَامِ وَٱلْحُرُمَـٰتُ قِصَاصٌ ۚ فَمَنِ ٱعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ فَٱعْتَدُوا۟ عَلَيْهِ بِمِثْلِ مَا ٱعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ ۚ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلْمُتَّقِينَ 194

{194} Yeye Mtukufu anasema: "Mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu." inawezekana kwamba kinachokusudiwa kwayo ni kile kilichotokea pale washirikina walipomzuia Nabii, – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, – na maswahaba wake katika mwaka wa Hudaybiyah; ili wasiingie Makka. Na wakadanganya suluhu kwamba wataingia humo mwaka uliofuata. Na kulikuwa kuzuilia huko katika mwezi mtukufu ambao ni Dhul-Qa`dah, kwa hivyo linakuwa hili kwa lile. Na ndani yake kuna kufurahisha nyoyo za maswahaba kwa kutimiza ibada yao na kuikamilisha. Na yawezekana kwamba maana yake kuwa mkiwapiga vita katika mwezi mtukufu, basi wao walikwisha pigana nanyi humo, na wao ndio walioanzisha. Basi hakuna ubaya wowote juu yenu katika hilo. Na kwa kuzingatia hilo, inakuwa kauli yake, “na vitu vitakatifu vimeekewa kisasi.” Ni katika mlango wa kuunganisha lililo la ujumla kwa lililo mahususi. Yani kila chenye kuheshimiwa kama vile mwezi mtakatifu, au mji mtakatifu, au ihramu, au lililo la ujumla zaidi kuliko hayo. Kila ambayo Sheria iliamrisha yaheshimiwe, basi mwenye kujasiri kulivunja, basi atafanyiwa kisasi. Na mwenye kupigana katika mwezi mtakatifu, yeye pia atapigwa (humo). Na mwenye kuukiuka mji mtakatifu, atafanyiwa adhabu ya Hadd (adhabu maalumu), na hana ulinzi katika mahali patakatifu. Na mwenye kumuua (mtu) aliye sawa na yeye, atauawa kwa ajili yake. Na atakayemjeruhi au kumkata kiungo chake, basi atalipizwa kisasi kwa ajili yake. Na atakayechukua mali ya mtu mwingine ambayo ni haramu kwake, itachukuliwa badala yake kutoka kwake. Lakini je, mwenye haki ana haki ya kuchukua kutoka katika mali yake kwa kiwango cha haki yake au hapana? Hili lina ikhtilafu baina ya wanachuoni. Na lililo sahihi zaidi katika kauli hizo ni kwamba ikiwa sababu ya kustahiki ni dhahiri, kama vile mgeni. Ikiwa hakuna mtu mwingine atakayemkaribisha isipokuwa yeye, na mke na jamaa. Ikiwa yule anayelazimika kuwatunza atakataa kuwapa matumizi, basi inaruhusika kuichukua kutoka katika mali yake. Na ikiwa sababu yake imefichika, kama vile mtu anayekanusha kuwa na deni la mtu mwingine. Au alimfanyia hiyana katika amana yake, au aliiba kutoka kwake, na mfano wa hayo, basi hairuhusiki kwake kuchukua katika mali yake ili kujilipa. Hili ni kwa ajili ya kupatanisha kati ya dalili hizi, na kwa sababu hiyo Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema akisisitiza na kuimarisha hayo yaliyotangulia. “Basi, anayewashambulia, nanyi mshambulieni kwa sawa na alivyowashambulia.” Huu ndio ufafanuzi wa namna ya kulipiza kisasi, na kwamba hiyo (namna) ndiyo iliyo sawa katika kukabiliana na mwenye kuanzisha uadui. Na kwa vile nafsi - katika hali nyingi - hazisimami katika mipaka yake ikiwa zimeruhusiwa kuadhibu kwa sababu ya kutaka kwake kupona. Yeye Mtukufu akaamrisha kudumu katika kumcha, ambako ndiko kusimamia kwenye mipaka yake, bila ya kuivuka. Na Yeye Mtukufu akajulisha kwamba Yeye kwa hakika yu “pamoja na wachamungu”. Yani kwa msaada, na nusura, na kuunga mkono, na kuwezesha. Na yule ambaye Mwenyezi Mungu yu pamoja naye, basi atapata furaha ya milele. Na yule asiyeshikamana na uchamungu, basi mlinzi wake atamwacha na asimsaidie, na amwachie nafsi yake. Basi maangamizo yake yatakuwa karibu zaidi naye kuliko mshipa wa shingo yake.