İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · Yunus
Sure 10

Yunus

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

Ayet 60

وَمَا ظَنُّ ٱلَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلْكَذِبَ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى ٱلنَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَشْكُرُونَ 60

{60} "Na ni nini dhana ya wale wanaomzulia Mwenyezi Mungu uongo Siku ya Qiyama?" Kwamba Mwenyezi Mungu atawaadhibu na kuwatesa. Yeye Mtukufu amesema, "Na Siku ya Qiyama utawaona wale waliomdanganyishia Mwenyezi Mungu nyuso zao zimefanywa kuwa nyeusi." "Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila juu ya watu" wengi, na mwenye wema mwingi, lakini wengi wa watu hawashukuru; ima kwa kutozishukuru hasa, au kwa kujisaidia kwazo katika kumuasi. Na ima waharamishe kwazo, au wakatae yale aliyowaneemesha kwayo Mwenyezi Mungu waja wake. Na ni wachache tu miongoni mwao wanaoshukuru ambao wanazikiri neema hizo, na kumsifu Mwenyezi Mungu juu yake, na kujisaidia kwazo katika kumtii. Na Aya hii inatumika kama ushahidi juu ya kanuni ya msingi katika vyakula vyote ni kwamba ni halali, isipokuwa vile ambavyo Sheria alikataza. Kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwakanusha wale wanaoharamisha riziki ambayo aliwateremshia waja wake.