Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-An'aam
Sura ya 6

Al-An'aam

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 3

وَهُوَ ٱللَّهُ فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَفِى ٱلْأَرْضِ ۖ يَعْلَمُ سِرَّكُمْ وَجَهْرَكُمْ وَيَعْلَمُ مَا تَكْسِبُونَ 3

{3} Yani Yeye ndiye anayefanyiwa uungu, anayeabudiwa "katika mbingu na katika ardhi." Basi wakazi wa mbinguni na ardhi wanamwabudu Mola wao Mlezi wakimnyenyekea kwa ukuu wake na wakimdhalilikia kwa nguvu yake na utukufu wake. Nao ni Malaika walio karibu na Mwenyezi Mungu, na Manabii, na Mitume, na wakweli, na Mashahidi, na wale walio wema. Naye Mtukufu "Anajua ya siri yenu na ya dhahiri yenu. Na anajua mnayoyachuma." Basi jihadharini na kumuasi na myatake zaidi matendo ambayo yatakayowaweka karibu naye, na yawatie karibu na rehema zake, na jihadharini na kila kitendo kitakachowaweka mbali naye, na mbali na rehema zake.