Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-An'aam
Sura ya 6

Al-An'aam

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 2

هُوَ ٱلَّذِى خَلَقَكُم مِّن طِينٍ ثُمَّ قَضَىٰٓ أَجَلًا ۖ وَأَجَلٌ مُّسَمًّى عِندَهُۥ ۖ ثُمَّ أَنتُمْ تَمْتَرُونَ 2

"Yeye ndiye aliyewaumba kutokana na udongo;" na hayo ni kwa asili yenu na baba yenu Adam, amani iwe juu yake. "Kisha akawahukumia muda;" yaani, aliweka kipimo kwa muda wa kukaa kwenu katika Nyumba hii mkistareheshwa, na kupewa mtihani, na kujaribiwa kwa yale Anayowatuma nayo Mitume Wake; ili awajaribu ni nani miongoni mwenu mwenye matendo mazuri zaidi, na awape umri wa kutosha mwenye ndani yake mwenye kukumbuka? "Na muda maalum uko kwake tu" nayo ni nyumba ya Akhera ambayo ataihamia mja kutoka katika Nyumba hii, na awalipe kwa matendo yao ya heri na maovu. "Kisha" baada ya ubainisho huu mkamilifu na kukata hoja; "Kisha nyinyi mnatia shaka," yaani, mnashuku katika ahadi ya Mwenyezi Mungu ya mema na ahadi yake ya adhabu, na kutokea kwa malipo Siku ya Kiyama. Na Mwenyezi Mungu alitaja giza kwa wingi kwa sababu ya wingi wa nyenzo zake na utofauti wa njia zake, na akaitaja nuru kwa umoja kwa sababu njia inayofikisha kwa Mwenyezi Mungu ni moja, na isiyo nyingi, nayo ni njia ile inayojumuisha kujua haki na kuifanyia kazi. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Na kwamba, kwa hakika hii ndiyo Njia yangu iliyoyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyinginezo, zikawatengenisha na Njia yake."