Al-Anbiyaa
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
لَوْ كَانَ فِيهِمَآ ءَالِهَةٌ إِلَّا ٱللَّهُ لَفَسَدَتَا ۚ فَسُبْحَـٰنَ ٱللَّهِ رَبِّ ٱلْعَرْشِ عَمَّا يَصِفُونَ 22
{22} Kwa hivyo mshirikina anaabudu kiumbe ambacho hakifaidishi wala hakidhuru, na anaacha kumkusudia Mwenyezi Mungu tu, ambaye ana ukamilifu wote na mikononi mwake ndiko kuna kuamrisha, kunufaisha, na kudhuru, na hii ni kutokana na ukosefu wake wa mafanikio, bahati mbaya, ujinga na ukali wa udhalimu wake. Haingii katika uwepo isipokuwa kwa Mungu mmoja; kama ambavyo haikupatikana ila kwa Mola mmoja tu, ndiyo sababu alisema: "Lau wangelikuwamo humo" mbinguni na ardhini, "miungu wengine isipokuwa Mwenyezi Mungu basi bila ya shaka hizo mbingu na ardhi zingelifisidika" katika dhati yake, na vikaharibika vilivyoko baina yake katika viumbe. Na maelezo ya hayo ni kwamba ulimwengu wa juu na wa chini kama unavyoonekana katika hali kamili zaidi ya utengenevu na mpangilio mzuri, ambao hauna dosari yoyote, wala kasoro, wala kukataa, wala pingamizi. Kwa hivyo hilo likaonyesha kwamba mwenye kuuendesha ni mmoja, na mlezi wake ni mmoja na Mungu wake ni mmoja. Na kama ulimwengu ungekuwa na waendeshaji wawili na mola wawili au zaidi, basi mfumo wake ungevurugika na nguzo zake zingeharibika. Kwa maana, wao wenyewe wataanza kuzuiana na kupingana. Na mmoja wao anapotaka kuendesha kitu, naye mwinginewe akataka kisitokee, basi jambo lisilowezekana kutokea wanayotaka hayo kwa pamoja, na kupatikana alichotaka mmoja wao pasi na alichotaka mwengineye ni ishara ya kushindwa kwa mwenginewe huyo, na kutoweza kwake, na kukubaliana kwao juu ya jambo moja katika mambo yote hakuwezekani. Basi inabakia tu kwamba Mshindi ambaye anafanya yapatikane makusudio yake Yeye peke yake bila ya mpingamizi yeyote wala mwenye kuzuia ni Mwenyezi Mungu, Mmoja, Mshindi. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akataja uthibitisho wa kutowezekana katika kauli yake, "Mwenyezi Mungu hakujifanyia mwana yeyote, wala hanaye mungu yeyote mwengine. Ingekuwa hivyo, basi kila mungu angelichukua alivyoumba, na baadhi yao wangeliwashinda wengine. Mwenyezi Mungu ametakasika mno na sifa hizo wanazomsifu kwazo." Na miongoni mwa hayo ni kama ilivyo katika moja ya tafsiri ya maneno yake Mtukufu, "Sema: Lau kuwa wangelikuwa pamoja naye miungu mingine kama wasemavyo, basi wangelitafuta njia ya kumfikia Mwenye Kiti cha Enzi." Subhanahu Wa Taa'la (Ametakasika na Ametukuka juu kabisa) na hayo wanayoyasema." Ndiyo sababu akasema hapa, "Subahana 'Llah (Ametakasika Mwenyezi Mungu)" kutokana na kila upungufu kwa sababu Yeye peke yake ndiye mkamilifu tu. "Bwana wa A'rshi (Kiti cha Enzi)" ambayo ndiyo dari ya viumbe, na ndiyo pana na kubwa zaidi kati yao. Kwa hivyo, kuwa kwake Bwana wa vinginevyo kunafailia zaidi "kutokana na hayo wanayoyazua" hao wanaomkataa na kumkufuru kama vile kumfanyia mwana na mke, kwamba ana mshirika kwa njia moja au nyingine.