Ash-Shams
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
وَٱلشَّمْسِ وَضُحَىٰهَا 1 وَٱلْقَمَرِ إِذَا تَلَىٰهَا 2 وَٱلنَّهَارِ إِذَا جَلَّىٰهَا 3 وَٱلَّيْلِ إِذَا يَغْشَىٰهَا 4 وَٱلسَّمَآءِ وَمَا بَنَىٰهَا 5 وَٱلْأَرْضِ وَمَا طَحَىٰهَا 6
{1 - 6} Mwenyezi Mungu Mtukufu aliapa kwa ishara hizi kubwa juu ya nafsi iliyofanikiwa na nafsi nyinginezo ambazo ni ovu, akasema: "Ninaapa kwa jua na mwangaza wake" na manufaa yake yatokayo humo. "Na kwa mwezi unapolifuatia" katika mashukio na nuru. "Na kwa mchana unapolidhihirisha!" Yaani unapodhihirisha na kuweka wazi vitu vilivyo juu ya uso wa ardhi. "Na kwa usiku unapolifunika." Yaani, unapofunika uso wa ardhi, kwa hivyo kila kilicho juu yake kinakuwa gizani. Basi mfuatano wa giza, nuru, jua na mwezi juu ya ulimwengu huu kwa mpangilio nzuri sana na kusimama sawaswa kwa masilahi ya waja ni ushahidi mkubwa zaidi kwamba Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi kila kitu, na ni Mwenye uwezo mno juu ya kila kitu, na kwamba Yeye pekee ndiye anayepasa kuabudiwa, ambaye kila kitu kingine kinachoabudiwa ni batili. "Na kwa mbingu na kwa aliyeijenga" Hapa inawezekana kwamba Mwenyezi Mungu aliapa kwa mbingu na aliyeijenga, ambaye ni Mwenyezi Mungu Mtukufu mwenyewe. Na inawezekana kwamba aliapa kwa mbingu na kujengwa kwake, ambako ndicho kipimo cha mwisho zaidi cha uundaji wa ustadi na uzuri. Na mfano wa hili ni kauli yake: "Na kwa ardhi na kwa aliyeitandaza" ili viumbe viweze kunufaika kwayo katika nyanja zote za manufaa.