At-Tawba
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِنَّمَا ٱلْمُشْرِكُونَ نَجَسٌ فَلَا يَقْرَبُوا۟ ٱلْمَسْجِدَ ٱلْحَرَامَ بَعْدَ عَامِهِمْ هَـٰذَا ۚ وَإِنْ خِفْتُمْ عَيْلَةً فَسَوْفَ يُغْنِيكُمُ ٱللَّهُ مِن فَضْلِهِۦٓ إِن شَآءَ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌ حَكِيمٌ 28
{28} Yeye Mtukufu anasema, "Enyi mlioamini! Hakika washirikina" wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu, wale walioabudu pamoja naye wengine "ni najisi." Yaani, wachafu katika itikadi zao na matendo yao. Na ni najisi gani iliyo kubwa zaidi kuliko yule anayeabudu miungu mingine pamoja na Mwenyezi Mungu, ambao hawafaidi wala hawadhuru wala hawamsaidii kitu. Na matendo yao ni kati ya kupigana na Mwenyezi Mungu na kuzuia njia ya Mwenyezi Mungu, na kunusuru batili na kuikataa haki, na kufanya uharibifu katika ardhi, siyo katika kufanya mambo yatengenee? Basi ni juu yenu kuisafisha Nyumba tukufu zaidi, na iliyo safi zaidi kutokana nao. "Kwa hivyo wasiukaribie Msikiti Mtakatifu baada ya mwaka wao huu." Nao ni mwaka wa tisa wa Hijra, wakati Abu Bakr As-Siddiq alipowaongoza watu katika Hijja, na Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie akamtuma binamu yake, Ali kwamba atangaze siku ya Hijja kubwa kujitenga mbali (kwa Mwenyezi Mungu na mtume wake na washirikina). Kwa hivyo akatangaza kwamba asihiji baada ya mwaka huu mshirikina yeyote, wala asiizunguke Nyumba Takatifu aliye uchi. Na kinachomaanishwa hapa si uchafu wa mwili, kwani makafiri, kama wengineo, ni wasafi wa kimwili, kwa ushahidi kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliruhusu kumjaamii mwanamke kutoka kwa watu wa Kitabu, na kumpapasa. Na wala hakuamrisha kuosha kile alichoshika katika mwili wake. Na Waislamu hawajaacha bado kushika mili ya makafiri, na wala haijawahi kuripotiwa kutoka kwao kwamba waliona kwamba ni miili michafu kama wanavyoona uchafu wa vitu najisi. Lakini kile kinachomaanishwa ni kama ilivyotanguliwa kwamba najisi yao ni najisi ya kimaana tu kwa sababu ya ushirikina. Kwa hivyo, kama vile kumpwekesha Mungu na kuwa na imani ni usafi, basi shirki ni najisi. Na kauli yake: "Na ikiwa mnahofia umasikini" na uhitaji kwa sababu ya kuwazuia washirikina kuukaribia Msikiti Mtakatifu, kwa hivyo yakakatika mahusiano yaliyo baina yenu na wao miongoni mwa mambo ya kidunia, "basi Mwenyezi Mungu atawatajirisha kutoka kwa fadhila yake akipenda;" kwa maana, riziki haikufungika katika mlango mmoja tu na pahali pamoja, lakini haufungiki mlango mmoja isipokuwa inafunguliwa milango mingi isiyokuwa huo. Kwa maana fadhila za Mwenyezi Mungu ni kunjufu, na ukarimu wake ni mkubwa, hasa kwa mwenye kuacha kitu kwa ajili ya Uso wake Mtukufu. Kwa maana Mwenyezi Mungu ndiye Mkarimu zaidi wa wakarimu wote. Na hakika Mwenyezi Mungu alitimiza ahadi yake; kwa maana Mwenyezi Mungu aliwatosheleza Waislamu kutoka katika fadhila zake, na akawakunjulia katika riziki ambazo kwazo walikuwa katika matajiri wakubwa zaidi na wafalme. Na kauli yake, "akitaka" ni kufungamanisha kutosheleza na kutaka kwake. kwa sababu kutosheleza katika dunia hii si katika matakwa ya imani, wala hakuonyeshi upendo wa Mwenyezi Mungu, ndiyo maana Mwenyezi Mungu akafungamanisha hilo na kutaka kwake. Kwani Mwenyezi Mungu humpa dunia hii ampendaye na asiyempenda, lakini hampi imani na Dini isipokuwa yule ampendaye. "Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima kubwa." Yaani, elimu yake ni kunjufu. Anajua yule ambaye unamfailia utajiri na yule ambaye haumfailii. Na anaviweka vitu pahali pake, na anaviteremsha katika vyeo vyake. Na inaonyesha Aya hii tukufu, ambayo ni kauli yake, "kwa hivyo wasiukaribie Msikiti Mtakatifu baada ya mwaka wao huu" kwamba washirikina baada ya kwamba waliokuwa wao ndio wamiliki na wakuu kwenye Nyumba Tukufu. Kisha uongozi wake ukawa ni wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na Waumini pamoja na kukaa kwao katika Nyumba hiyo, na Makka, kisha aya hii ikateremka. Na Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alipokufa, aliamrisha kwamba waondolewe kutoka Hijaz, ili kusibakie dini mbili ndani yake. Na haya yote ni kwa ajili ya kumweka mbali kila kafiri na Msikiti Mtakatifu. Kwa hivyo hilo linaingia katika kauli yake, "kwa hivyo wasiukaribie Msikiti Mtakatifu baada ya mwaka wao huu."