Al-Jaathiya
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
وَلَقَدْ ءَاتَيْنَا بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ ٱلْكِتَـٰبَ وَٱلْحُكْمَ وَٱلنُّبُوَّةَ وَرَزَقْنَـٰهُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَـٰتِ وَفَضَّلْنَـٰهُمْ عَلَى ٱلْعَـٰلَمِينَ 16
{16} Yaani, tuliwaneemesha Wana wa Israili neema ambazo hawakuwahi kupewa wasiokuwa wao miongoni mwa watu, na tukawapa "Kitabu;" yaani, Taurati, Injili, kuhukumu baina ya watu, na unabii waliokuwa tofauti sana na watu wengine. Na unabii huo ukawa katika kizazi cha Ibrahim, amani iwe juu yake, ambao wengi wao walikuwa katika Wana wa Israili. "Na tukawaruzuku vitu vizuri vizuri" kama vile vyakula, vinywaji na mavazi, na tukawateremshia Manna na Salwa. "Na tukawafadhilisha kuliko walimwengu wote." Yaani, juu ya viumbe wengineo kwa neema hizi. Ila umma huu unatoka katika ujumla huu wa kimatamshi, kwani wao ndio umma bora kabisa uliowahi kutolewa kwa ajili ya watu. Na muktadha unaonyesha kwamba kinachokusudiwa ni kingine kisichokuwa umma huu. Kwa sababu Mwenyezi Mungu anatusimulia yale aliyowaneemesha kwayo Wana wa Israili na akawatofautisha na watu wengine (wa zama zao). Na pia, fadhila ambazo kwazo Wana wa Israili walifanywa kuwa bora ni kama vile Kitabu, hekima, Unabii na sifa nyinginezo zote zinazopatikana katika umma huu, na umma huu ukawazidi kwa fadhila nyingi sana. Kwa maana, sheria ya Wana wa Israili ni sehemu katika sheria hii. Kwa maana Kitabu hiki ndicho kinachotawala vitabu vyote vilivyotangulia, naye Muhammad – rehema na amani ziwe juu yake – anawasadikisha Mitume wote.