Aller au contenu
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Ghaafir
Sourate 40

Al-Ghaafir

Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.

Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22

Verset 29

يَـٰقَوْمِ لَكُمُ ٱلْمُلْكُ ٱلْيَوْمَ ظَـٰهِرِينَ فِى ٱلْأَرْضِ فَمَن يَنصُرُنَا مِنۢ بَأْسِ ٱللَّهِ إِن جَآءَنَا ۚ قَالَ فِرْعَوْنُ مَآ أُرِيكُمْ إِلَّا مَآ أَرَىٰ وَمَآ أَهْدِيكُمْ إِلَّا سَبِيلَ ٱلرَّشَادِ 29

{29} Kisha akawaonya watu wake, akawanasihi, akawahofisha juu ya adhabu ya Akhera na akawakataza wasidanganywe na ufalme wa dhahiri. Akasema: "Enyi watu wangu! Leo mna ufalme" katika dunia hii, "mmeshinda katika nchi" juu ya watu walio chini ya utawala wenu, mnawaendesha mtakavyo. Basi chukulieni kwamba hayo yote mnayo nyinyi na yalitimia, lakini hayawezi kutimia. "Basi ni nani atakayenisaidia kutuokoa na adhabu ya Mwenyezi Mungu kama ikitufikia?" Hili ni katika njia yake nzuri ya kulingania kwa Mwenyezi Mungu, ambapo aliwaingiza katika jambo hili na pia akajiingiza humo yeye mwenyewe aliposema: "Kama ikitufikia," ili awafahamishe kuwa anawanasihi na pia anajinasihi yeye mwenyewe, na anawapendelea yale anayoipendelea nafsi yake. "Firauni akasema" akimpinga katika hayo na kuwahadaa watu wake ili wasimfuate Musa: "Sikupeni shauri ila ile niliyoiona, wala sikuongozeni ila kwenye njia ya uwongofu." Naye alikuwa mkweli katika kauli yake: "Sikupeni shauri ila ile niliyoiona." Lakini aliona nini? Aliona kwamba awachezee watu wake ili wamfuate na ili aweze kusimamisha uongozi wake kwa hao. Na wala hakuona kwamba yeye yuko kwenye haki, bali aliona kwamba haki iko upande wa Musa na akaiikataa hali ya kuwa nafsi yake ina yakini nayo. Naye alidanganya katika kauli yake: "Wala sikuongozeni ila kwenye njia ya uwongofu." Huku ni kupindua uhakika wa mambo. Kwani, kama angewaamrisha wamfuate tu katika ukafiri wake na upotofu wake, basi uovu wa hilo ungekuwa mdogo zaidi. Lakini aliwaamrisha kumfuata na akadai kuwa kumfuata ndio kufuata haki, na kwamba kufuata haki ndiyo kufuata upotofu.