An-Nisaa
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
فَإِذَا قَضَيْتُمُ ٱلصَّلَوٰةَ فَٱذْكُرُوا۟ ٱللَّهَ قِيَـٰمًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِكُمْ ۚ فَإِذَا ٱطْمَأْنَنتُمْ فَأَقِيمُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ ۚ إِنَّ ٱلصَّلَوٰةَ كَانَتْ عَلَى ٱلْمُؤْمِنِينَ كِتَـٰبًا مَّوْقُوتًا 103
{103} Yani mtakapoimaliza Swala yenu, Sala ya hofu na nyinginezo, basi mkumbukeni Mwenyezi Mungu katika hali zenu zote, na namna zenu. Lakini hilo ilifanywa kuwa mahususi kwa swala ya hofu kwa faida mbalimbali: Miongoni mwake ni kwamba kutengenea kwa moyo, na kufaulu kwake, na furaha yake huja kwa kumrudia Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa upendo na kuujaza moyo na ukumbusho wake na kumsifu. Na kubwa zaidi lenye kufanikisha lengo hili ni swala, ambayo uhakika wake ni kwamba ni kiunganisho kati ya mja na Mola wake Mlezi. Na miongoni mwake ni kwamba ndani yake kuna hakika za imani na maarifa ya yakini yaliyolazimu kwamba Mwenyezi Mungu aiwajibishe kwa waja wake kila mchana na usiku. Na inavyojulikana ni kuwa makusudio haya yenye kusifiwa hayafikiwi katika sala ya hofu kwa sababu ya kushughulika kwa moyo na mwili, na hofu. Kwa hivyo akaamrisha yalipwe hayo kwa ukumbuko baada yake. Na miongoni mwake ni kwamba hofu husababisha moyo kuwa na wasiwasi na woga, jambo ambalo lina uwezekano mkubwa kumfanya uwe na udhaifu. Na moyo unapokuwa dhaifu, mwili unakuwa dhaifu juu ya kumpinga adui. Na kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kufanya hilo kwa wingi ni katika makubwa zaidi miongoni mwa yale yanayouimarisha moyo. Na miongoni mwake ni kwamba kumkumbuka Mwenyezi Mungu pamoja na subira na uthabiti ni sababu ya kufaulu, na ushindi dhidi ya maadui. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, “Enyi mlioamini! Mnapokutana na kundi (la kijeshi), basi kueni imara, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu sana ili mfanikiwe.” Kwa hivyo akaamrisha kulifanya hilo kwa wingi katika hali hii, pamoja na hukumu nyinginezo. Na kauli yake, “Na mtakapotulia, basi simamisheni Swala.” Yani mnapokuwa mmesalimika kutokana na hofu, na nyoyo zenu na miili yenu vikatulia, basi isimamisheni swala yenu kwa namna kamilifu kabisa, kwa nje na ndani, kwa nguzo zake, na masharti yake, unyenyekevu wake, na yote yenye kuikamilisha. “Kwani hakika Swala juu ya Waumini ni andiko lililowekewa nyakati maalum.” Yani imefaradhishwa katika wakati wake. Na hilo linaashiria ufaradhi wake, na kwamba ina wakati ambao haifai isipokua katika huo tu. Nazo ni hizi nyakati ambazo Waislamu walikwisha zijua, wadogo wao na wazee wao, wasomi wao na wajinga wao. Nao walichukua hilo kutoka kwa Nabii wao Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – aliposema, “Swalini kama mlivyoniona nikiswali.” Na iliashiria kauli yake, "Juu ya Waumini" kwamba sala ni mizani ya imani, na kulingana na imani ya mja, inakuwa sala yake, inatimia na inakamilika. Na hilo linaashiria kuwa makafiri - hata wakishikamana na hukumu za Waislamu, kama vile watu wa Dhimma – hawazungumzishwi kuhusu matawi ya dini, kama vile swala, na wala hawaamrishwi kuyafanya. Bali hata hayawi sahihi kutoka kwao maadamu wanaendelea na ukafiri wao, licha ya kwamba wataadhibiwa juu yake, na juu ya hukumu zote katika Akhera.