Yaseen
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
وَمَا لِىَ لَآ أَعْبُدُ ٱلَّذِى فَطَرَنِى وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ 22 ءَأَتَّخِذُ مِن دُونِهِۦٓ ءَالِهَةً إِن يُرِدْنِ ٱلرَّحْمَـٰنُ بِضُرٍّ لَّا تُغْنِ عَنِّى شَفَـٰعَتُهُمْ شَيْـًٔا وَلَا يُنقِذُونِ 23 إِنِّىٓ إِذًا لَّفِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ 24 إِنِّىٓ ءَامَنتُ بِرَبِّكُمْ فَٱسْمَعُونِ 25
{22 - 25} Ni kana kwamba watu wake hawakukubali nasaha yake, bali walimlaumu kwa kuwafuata Mitume hao na kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake katika Dini. Basi akasema: "Na kwa nini nisimuabudu yule aliyeniumba na kwake nitarejeshwa?" Kwani yeye ndiye anayestahiki kuabudiwa, kwa sababu Yeye ndiye aliyeniumba, na akaniruzuku, na kwake Yeye ndiye marejeo ya viumbe vyote. Kwa hivyo Yule ambaye mkononi mwake ndiko kuko kuumba, kuruzuku na kuhukumu baina ya waja duniani na akhera ndiye anayestahiki kuabudiwa, kusifiwa, na kuhimidiwa na si yule ambaye hamiliki manufaa wala madhara wala kupeana wala kuzuia wala mauti wala uhai wala kufufua. Ndiyo maana akasema: "Je, niishike miungu mingine badala yake? Arrahmani (Mwingi wa Rehema) akinitakia madhara uombezi wa hao hautanifaa kitu," kwa sababu hapana anayeweza kufanya uombezi kwa Mwenyezi Mungu ila kwa idhini yake. Kwa hivyo, uombezi wa hao hautanifaa kitu "wala hawataniokoa" kutokana na madhara ambayo Mwenyezi Mungu alinitakia. "Basi hakika mimi hapo" ikiwa nikiwaabudu miungu ambao hizi ndizo sifa zao "nitakuwa katika upotovu ulio dhahiri." Basi akaunganisha katika maneno haya kati ya kuwanasihi na kuwashahidilia Mitume hao kwamba ni Mitume, na kwamba ni waongofu. Na kujulisha kwamba Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anayestahiki kuabudiwa, na akataja ushahidi juu ya hayo, na kwamba kumuabudu asiyekuwa Yeye ni batili, na akataja ushahidi wa hilo, na akajulisha kwamba wenye kuabudu wasiokuwa Mwenyezi Mungu ni wapotofu, na kutangaza imani yake hadharani pamoja na kuhofu sana kwamba wanaweza kumuua. Alisema: "Hakika mimi nimemuamini Mola wenu Mlezi, basi nisikilizeni!"